Home Habari za michezo DR SAMIA AENDELA KUIBEBA YANGA CAF…PAMOJA NA TIKETI 5000, AHADI YAKE MPYA...

DR SAMIA AENDELA KUIBEBA YANGA CAF…PAMOJA NA TIKETI 5000, AHADI YAKE MPYA HII HAPA…

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amenunua tiketi 5000 kuelekea mchezo wa fainali ya kombe la shirikisho Afrika kati ya Yanga na USM Algers utakaopigwa Mei 28 katika dimba la Benjamini Mkapa.

Akiwasilisha ahadi hiyo ya Rais Msemaji wa Serikali Gerson Msigwa amesema lengo la Rais Samia ni kutengeneza mazingira mazuri kwa Yanga kutwaa ubingwa wa shirikisho Afrika na kuandika historia mpya kwenye soka la Tanzania.

Aidha Msigwa amesema Rais Samia amewataka wadau wengine kujitokeza kununua tiketi kwa ajili ya mchezo huo ili kuwapa nafasi mashabiki wengi zaidi kuhudhuria mchezo huo na Yanga kuutumia vyema uwanja wa nyumbani kwa nguvu ya mashabiki.

Hii inakuja baada ya hivi karibuni pia Serikali yake kuhaidi kutoa ndege ya kuipeleka timu Algeria na kuwarudisha baada ya mechi ambapo macho na matarajio ya Watanzania wengi nikuona Yanga wakirudi Tanzania na Ubingwa huo.

Hii sio mara ya kwanza kwa Dr Samia kutoa sapoti kwenye masuala ya michezo kwani amekuwa akizipa hamasa Simba na Yanga kwenye mashindano ya kimataifa ambapo alianza kwa kununua magoli kuanzia hatua ya Makundi mpaka sasa Yanga walipoingia Fainal.

Kitendo cha Yanga kuingia Fainal kinaonyesha mafanikio makubwa ambayo yamepatikana kwenye michezo toka aingie madarakani mwaka 2021.

Rais Samia amekuwa mzalendo na mwenye mapenzi makubwa na sekta ya michezo nchini, ambapo sapoti yake haijaishia tu kwenye mchezp wa  soka bali imegusa karibu michezo yote.

SOMA NA HII  CV YA KOCHA MPYA WA VIUNGO YANGA HII HAPA