Home Uncategorized KAGERA SUGAR: BADO TUPO SOKONI KUSAKA MAJEMBE

KAGERA SUGAR: BADO TUPO SOKONI KUSAKA MAJEMBE

MECKY Maxime amesema kuwa kwa sasa tayari amefanikiwa kufanya usajili kwa wachezaji aliokuwa anawahitaji hivyo ni nafasi chache zimebaki.

Maxime amesema kuwa msimu ujao anahitaji kuleta ushindani mkubwa na anaamini kwa usajili ambao wameufanya watafanya vizuri.

“Hatuna tatizo kubwa kwa sasa kwani kwa asilimia kubwa tumekamilisha usajili kwa wachezaji ambao tulikuwa tunahitaji kuwapa kandarasi, ni nafasi chache ambazo zimebaki hivyo muda si mrefu tutakamilisha kazi yetu,” amesema.

Miongoni mwa nyota ambao wamesajiliwa ni pamoja na Evarigitius Mujwahuki ambaye amesaini kandarasi ya mwaka mmoja akitokea Mbao FC pamoja na Benedict Tinnoco mlinda mlango aliyetokea Mtibwa Sugar.

SOMA NA HII  HAPA SIMBA,PALE YANGA, HUKU HESHIMA PALE REKODI SIO POA HUKO LIGI YA MABINGWA