Home Uncategorized KASSIM KHAMIS, IDDY SULEIMAN WAMPA WAKATI MGUMU NYOTA AZAM FC

KASSIM KHAMIS, IDDY SULEIMAN WAMPA WAKATI MGUMU NYOTA AZAM FC


KUSAJILIWA kwa nyota wa Mbeya City FC, Iddy Suleiman, Kassim Khamis kutoka Kagera Sugar kumefanya nafasi ya mshambuliaji Mbaraka Yusuph kuwa finyu hali inayowafanya mabosi hao kufikikria kumtoa kwa mkopo Mbaraka Yusuph.


Yusuph alitolewa kwa mkopo Namungo FC na tayari amemaliza mkataba wake kwa sasa amerejea Bongo akiisubiri timu irejee kutoka Rwanda ambao inashiriki michuano ya Kagame na leo inacheza fainali.

Habari zinaeleza kuwa kwa sasa mabosi wa Azam FC wanafikiria kumtoa kwa mkopo kumrejesha Kagera Sugar mchezaji huyo ili alinde kipaji chake jambo ambalo Yusuph kaligomea.

“Mimi ni mchezaji wa Azam kwa kuwa nimemaliza mkataba wa kuitumikia Namungo, ishu ya kutolewa kwa mkopo tena sijaipata kwa sasa ninachojua msimu ujao nitakuwa ndani ya Azam FC,” amesema. 
SOMA NA HII  HAJI MANARA AMZUNGUMZIA JACKLINE WOLPER