Home Uncategorized YANGA MPYA YANGA ATAJA SIKU YA KUTUA BONGO

YANGA MPYA YANGA ATAJA SIKU YA KUTUA BONGO


 FAROUK Shikalo mlinda mlango wa Yanga amesema kuwa kwa sasa hana taabu yoyote kujiunga na mabosi hao anachosubiri ni simu tu atie timu Bongo siku yoyote kuanzia sasa.


Nyota huyo alikuwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Kenya, Harambee Stars iliyokuwa ikishiriki michuano ya Afcon iliyomalizika jana na alikuwa na klabu yake ya Bandari iliyokuwa ikishiriki michuano ya Kagame na imeshatolewa.

Shikalo amesema kuwa anamalizia mapumziko yake na muda si mrefu atatua Bongo akipigiwa simu na mabosi wake wa Yanga.

“Nipo nyumbani Kenya kwa mapumziko, ilikuwa ni muhimu kuiona familia ila kwa sasa nasubiria viongozi wa Yanga tu wanipe ratiba ya kushuka Bongo nianze kazi,” amesema.

Mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh amesema kuwa muda wowote mlinda mlango huyo atatua Bongo kwani alipewa mapumziko.
SOMA NA HII  YANGA NOMA YATAWALA KIKOSI CHA KWANZA, MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATANO