Home kimataifa KUMBE RAMOS KUTOITWA TIMU YA TAIFA IMEMUUMA

KUMBE RAMOS KUTOITWA TIMU YA TAIFA IMEMUUMA


BAADA ya Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Hispania Luis Enrique kupanga kikosi chake cha timu ya Taifa ya Hispania kuelekea michuano ya Euro 2020 inayotarajiwa kuanza Juni 11, 2021 huku akimtema nahodha wa timu hiyo, Sergio Ramos nyota huyo amesema kuwa ameumia.

 Kwenye orodha ya wachezaji 24 walioitwa mbali na Ramos kutemwa hakuna hata jina moja la mchezaji wa Real Madrid inayoshiriki La Liga.

Ramos ambaye alikuwa ni nahodha wa timu ya taifa ya Hispania amesema:-“Baada ya msimu mrefu wa mapambano na ugumu nakiri kuwa nimepitia mengi magumu na hili la Euro linaingia.

“Nimepambana kama ilivyo siku zote kwa mwili na nafsi yangu ili nirejee kwenye ubora wangu kwa 100% kwa ajili ya klabu na timu yangu ya taifa ila sio kila muda mambo huwa vile tunadhani.


“Imeniuma sikuweza kuisaidia Real Madrid na kuipambania timu yangu ya taifa, lakini sina budi kupumzika ili kurejea vyema kwa ajili ya klabu na Taifa langu.


“Kutoka moyoni nawatakia kheri Wachezaji wenzangu wa timu ya taifa, nami nitakuwa nyumbani kuishangilia timu kama watu wengine, kila la kheri Hispania,” amesema Sergio Ramos, Nahodha wa Real Madrid.

SOMA NA HII  ISHU YA KANE KUSEPA SPURS BADO NGOMA NZITO