Home Habari za michezo ‘KITANZI’ CHA SIMBA NA YANGA KUFUNGWA KWA MKAPA….CAF KUHUSIKA A-Z…..

‘KITANZI’ CHA SIMBA NA YANGA KUFUNGWA KWA MKAPA….CAF KUHUSIKA A-Z…..

Habari za michezo

Makosa ya waamuzi wa Ligi Kuu Bara yanaweza kuanza kupungua siku chache zijazo kufuatia taarifa njema ya kufungwa kwa teknolojia ya usaidizi wa video kwa waamuzi wa soka (VAR), zoezi ambalo mchakato wake unatarajia kuanza hivi karibuni.

Hiyo ni kufuatia uamuzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), kuipa Tanzania vifaa vya VAR ambavyo vitafungwa katika baadhi ya viwanja.

Akizungumza jana Jumamosi Desemba 16, 2023 katika mkutano mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) unaofanyika Iringa, Rais wa shirikisho hilo, Wallace Karia amesema ufungwaji wa vifaa hivyo utafanywa katika viwanja vinavyokidhi vigezo vya CAF na shirikisho la mpira wa miguu duniani (FIFA).

“Niwape habari njema kuwa tumepata VAR kutoka CAF na hii ni muendelezo wa uhusiano mzuri na CAF. Wataalam wameingia jana kutoa mafunzo. Itafungwa katika viwanja vyenye ‘standard’ (ubora).

“Kamati ya waamuzi kwa vile tumewapa jukumu la usimamizi mtasaidia katika mafunzo na uzuri tunaye mkufunzi wa waamuzi wa CAF, Leslie Liunda ambaye atakuwa mratibu wa hayo mafunzo,” alisema Karia.

Karia alisema kuwa wanaangalia pia uwezekano wa VAR kufungwa katika Uwanja wa Amaan Zanzibar.

SOMA NA HII  JINYAKULIE MAPESA KEDEKEDE KUPITIA SLOT YA TITAN DICE KUPITIA MERIDIANBET CASINO