Home Infinix MALIZA MWAKA KWA ‘UTASHA’ BOMBA WA Infinix HOT 40 PRO….KUIPATA NI MTELEZO...

MALIZA MWAKA KWA ‘UTASHA’ BOMBA WA Infinix HOT 40 PRO….KUIPATA NI MTELEZO TU….

Infinix

Kampuni ya simu za mkononi Infinix Tanzania imezidua simu mpya ambayo itakuwa msada kwa kijana ambaye kwake simu ni kama Ofisi, Infinix HOT 40 pro imeonekana kuvutia wasanii wengi ikiwemo mtengenezaji wa music Video Director Nicklass pamoja na msanii wa Music wa kizazi kipya almaarufu Quick Rocka wote wakionekana kuvutiwa na Processor ya G99 iliyopo katika simu hiyo namna inavyoendesha application kama za gaming na nyenginezo kwa haraka.

Wakati wa uzinduzi na vyombo vya habari, Quick Rocka, alielezea kufurahishwa kwake na utendakazi wa kipekee pamoja na muonekano wa simu hiyo.

Alisema “HOT 40 Pro ina kichakataji cha Helio G99, inafanya kazi kwa kasi na kufanya mchakato mzima wa utumiaji simu kuwa mwepesi na wa haraka, mfumo wake wa kuchaji ni haraka simu hii ina Watt33 teknolojia hii bunifu huwezesha watumiaji kuchaji betri kutoka 20% hadi 75% kwa dakika 35 tu na uhakikisha usalama na maisha marefu ya betri kwa hadi miaka 4”.

InfinixDirector Nicklass nae alionekana kukoswa na camera za simu hiyo alisema kuwa, teknolojia kweli imekuwa kubwa simu hii inachukua matukio kwa camera zote mbili kwa wakati mmoja. Wapenda Selfie na wapenzi wa picha kali ina kamera kuu ya 108MP yenye kihisi cha HM6, kinachohakikisha kuwa picha kali na za wazi zenye pikseli 0.64-micron, hata baada ya kupunguzwa/cropping.

Lenzi kuu ya 2MP hunasa picha za karibu za maumbo na maelezo tata. Kamera ya mbele iliyoboreshwa ya 32MP AI hutoa picha za kipekee za kikundi na selfies, hata katika mwanga hafifu, shukrani kwa flash yake ya juu ya mbele.”

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mtaalamu wa Bidhaa wa Tigo, Lilian Mushi alisema “Sisi Tigo Tanzania tunayofuraha kushirikiana na Infinix katika uzinduzi wa toleo la HOT 40, ambayo ni hatua muhimu katika kufafanua upya uzoefu wa michezo kwa simu za mkononi.

Sisi kama washirika wa mawasiliano ya simu, tunafuraha. ili kuwapa wateja wa Tigo muunganisho usio na matatizo ili kufurahia kikamilifu uwezo wa game za simu ulioimarishwa na simu za toleo la HOT 40.

Vipengele/features vya kisasa vya HOT 40 Pro, pamoja na mtandao wa Tigo wa kutegemewa wa 4G+ na 5G, huhakikisha kwamba watumiaji wanaweza kujiingiza katika michezo ya simu na burudani.Tunatambua HOT 40pro na HOT 40i kama uthibitisho wa kujitolea kwa Infinix katika kusukuma mipaka katika teknolojia na ubunifu, sisi kama Tigo Tanzania tunatoa bando la intaneti la GB 78 kwa wateja wa HOT 40.”

InfinixHaikuishia hapo Infinix ilipata wasaa pia wakutuhabarisha kuhusu ushirika wake na FREE FIRE, ushirikiano kati ya Infinix na Free Fire huongeza zaidi burudani ya michezo ya simu na kutoa uzoefu wa kusisimua na wa ushindani wa michezo kupitia simu kwa watazamaji.

Uzinduzi huo ulienda sambamba na mobile game, ambapo gamers walichuana vikali kwa kuchezesha games la Free Fire na katika mashindano hayo ushindi mkubwa ulienda kwa kikundi kinachofahamika kama maza fanta ambao walijinyakulia kitita cha shillingi 1M na Infinix HOT 40 pro kwa kila mwanakikundi.

Infinix HOT 4O pro na HOT 4Oi zimeanza kupatikana nchi nzima lakini pia usikose kununua matoleo mengine ya Infinix katika msimu huu wa sikukuu ya Christmass na Mwaka Mpya promosheni ya #kubwayamoto imeshaanza na wateja kujishindia mamilioni ya zawadi ikiwemo pikipik, laptop na simu za Infinix.

Tembelea @infinixmobiletz kujua zaidi kuhusiana na habari hii.

SOMA NA HII  UKWELI WA MAMBO....KWA SIMBA HII ..UKIJICHANGANYA TU..IMEKULA KWAKO MAZIMA...