Home Simba SC ALICHOKISEMA HANS POPE BAADA YA MANARA ‘KUBANDULIWA’ MSIMBAZI

ALICHOKISEMA HANS POPE BAADA YA MANARA ‘KUBANDULIWA’ MSIMBAZI


BAADA ya Simba SC kutwaa ubingwa mara mbili mfululizo katika Kombe la FA, huku wakiitawala Ligi Kuu kwa kutwaa makombe kwa misimu manne mfululizo pamoja na Haji Manara kubwaga manyanga Simba, Mjumbe wa Bodi ya Utendaji ya Simba Zakaria Hans Pope ameibuka na kusema kuwa sasa mipango yao yote ni kuchukua ubingwa  katika michezo ya kimataifa.

Simba imefanikiwa kufikisha idadi ya ubingwa mara nne mfululizo katika Ligi Kuu Bara hadi sasa pia imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Shirikisho la Azam mara tatu.

Akizungumzia mipango yao, Hans Pope amesema kuwa kwa ubingwa walionao sasa unatosha kudhidirisha kuwa wao ndio mabingwa wa nchi, na wanahitaji kupata ubingwa huo hata katika michezo ya kimataifa.

“Simba ni timu kubwa kwa sasa na ndio mabingwa wa nchi kwa kuwa tumeshachukua makombe ya Ligi Kuu mara nne, na sasa tumechukua Kombe la FA kwa mara ya tatu tayari inatosha kuonyesha ukubwa wetu.

“Tunachokitaka kwa sasa ni kuvuka mipaka na kuchukua ubingwa katika mashindano mbalimbali ya kimataifa tumeshachukua sana huku nyumbani, na tumezoea ubingwa wa nyumbani hivyo kwa sasa ni levo nyingine za kimataifa na kuonyesha ukubwa wa Simba,”amesema Hans Pope.

SOMA NA HII  CHILUNDA APEWA MTIHANI HUU NA UONGOZI WA SIMBA