Home Habari za michezo DABI YA KARIAKOO NGUMU KUMEZA,MANARA APATA KIGUGUMIZI

DABI YA KARIAKOO NGUMU KUMEZA,MANARA APATA KIGUGUMIZI

HAJI MANARA AUMBUKA...NI BAADA YA KUMGOMBANISHA RAISI YANGA NA MTANGAZAJI

Aliyekuwa msemaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara amesema kuwa ni ngumu kutabiri matokeo ya mchezo wa Dabi kati ya Simba na Yanga kwani mchezo huo una mambo mengi nje ya uwanja tofauti na michezo mingine.

Manara amesema hayo kuelekea mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kati ya watani hao wa jadi utakaopigwa Jumapili ijayo katika Dimba la Mkapa.

“Haijawahi kuwa mechi rahisi zinapocheza Yanga na Simba, na kutabiri matokeo unaweza kiuchawi au kibetting, ila kujua matokeo halisi haiwezekani.

“Huwezi jua nani atashinda au kufungwa hata kama timu moja ipo katika mazingira rafiki zaidi ya kushinda hiyo mechi. Pamoja na hayo karata yangu nawapa nafasi kubwa ya Yanga kushinda kwa sababu za kiufundi zaidi.

“Ili Yanga wafungwe itabidi wafanye makosa mengi mno katika defence line yao, otherwise ule utatu wa Maxi Nzengeli, Pacome Zouzoua na Aziz KI unakwenda kumaliza mechi mapema,” amesema Manara.

SOMA NA HII  AHMED ALLY AWATULIZA MASHABIKI WA SIMBA