Home Habari za michezo WATAKAOENDA KUTAZAMA KOMBE LA DUNIA QATAR WAZUIWA KUFANYA NGONO NA KUNYWA POMBE…ADHABU...

WATAKAOENDA KUTAZAMA KOMBE LA DUNIA QATAR WAZUIWA KUFANYA NGONO NA KUNYWA POMBE…ADHABU NI JELA AU KIFO…


FIFA imetoa onyo ya kuwa mbinu kali zitatumika kuzuia vitendo vya kufanya mapenzi katika mashindano ya mwaka huu ya Kombe la Dunia yanayoenda kufanyika kwenye nchi ya kiarabu yenye sheria kali.

Vitendo vyote vya kufanya mapenzi kati ya watu ambao si wanandoa havitovumilika.

“Ufanyaji mapenzi kiholela umepigwa marufuku kwenye Kombe la Dunia la mwaka huu. Mashabiki mnaombwa kujiandaa. Kila mmoja atatakiwa kujilinda mwenyewe.”

Nchini Qatar ufanyaji wa mapenzi nje ya ndoa hukumu yake ni kifungo cha jela kinachoweza kufikia miaka 7.

Mashabiki wanakumbushwa kwamba japokuwa pombe si kinyume na sheria nchini humo, hairuhusiwi kabisa kunywa hadharani na pia kulewa hadharani ni kosa.

Kingine ni kuwa yoyote atakayekutwa akitumia dawa za kulevya aina ya cocaine hukumu yake ni kifo.

SOMA NA HII  ACHANA NA JEZI YAKE NO 6....HII HAPA REKODI YA KIBABE ILIYOWEKWA NA 'SKUDU' NDANI YA TZ...