Home Habari za michezo YANGA WAPANIA….WAANZA KUIBOA SIMBA TARATIIBUUU…ISHU YA ONYANGO KUJIUNGA NAO NI SUALA LA...

YANGA WAPANIA….WAANZA KUIBOA SIMBA TARATIIBUUU…ISHU YA ONYANGO KUJIUNGA NAO NI SUALA LA MUDA TU…


YANGA imepania kusuka ukuta mpya tayari kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa.

Sasa inasaka beki wa kati na hesabu yao ya kwanza ni beki mwili nyumba wa Simba, Joash Onyango.

Inafahamika tayari Yanga wamesharusha ndoano na anayesubiriwa ni Mkenya huyo tu kufanya uamuzi wa mwisho.

Lakini hesabu ya pili ya Yanga endapo watamkosa Onyango, ipo nchini Ghana na pale wanafanya mazungumzo na beki mmoja wa kati Yussif Mubarik ambaye anaitumikia klabu ya Asante Kotoko.

Mubarik ambaye anapendelea kunyoa panki ni msimu wa pili sasa yuko katika kiwango bora na takwimu zake za ubora zimewafanya mabosi wa Yanga kushawishika ili aje kuimarisha safu yao ya ulinzi zaidi. Beki huyo mrefu mwenye hesabu nzuri katika kuwazima washambuliaji pia amekuwa bora kwa mipira ya juu ubora ambao Kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi amekuwa akisisitiza anataka mwanaume wa kazi hiyo.

Mapema mabosi wa Yanga walishamshika kitasa wa Simba Joash Onyango ambaye mkataba wake na Simba unafikia tamati mwisho wa msimu.

Yanga walimpa kazi moja Onyango ataje yeye kiasi anachotaka lakini bado anajivutavuta, ingawa habari za ndani zinasema anasikilizia Simba watakuja na ofa gani lakini Yanga wameshtukia hilo na kuanza mazungumzo na Mubarik fasta ambaye muda wowote lolote linaweza kutokea.

Beki huyo ana mawasiliano ya karibu na meneja wa mshambuliaji wa timu hiyo, Yacouba Songne ambaye ndiye amepewa kazi ya kusuka dili hilo na kuhakikisha kila kitu kinakaa sawa na yeye amewahakikishia kijana hana noma.

“Ni beki mzuri anajua kuanzisha mashambulizi na umiliki wake wa mpira ni wa kiwango kikubwa kama tutampata tutakuwa tumelamba dume sana,” alisema bosi mmoja wa Yanga.

Habari za uhakika kutoka Yanga zinasema viongozi wengi wa usajili wanashawishi kuachana na Onyango na kubeba Mghana huyo kutokana na ishu ya umri na umakini ingawa wengine wanadai Onyango ni mzoefu na si msumbufu.

Habari zinasema Onyango amewaambia Yanga atasaini wasiwe na presha, ingawa wenyewe wameamua kujiongeza kutokana na hali halisi ya klabu hizo huku kukiwa na habari Simba watamwongezea mkataba na hawawezi kumuacha aondoke.

SOMA NA HII  YANGA WAENDELEA KUWABAKISHA MASTAA WAO...LEO ZAMU YA ZAWADI MAUYA...ASAINI MKATABA MPYA WA MAMILIONI YA PESA...