Home Uncategorized KIUNGO POLISI TANZANI- NIYONZIMA AMENIIBA NAFASI YANGU YA KUSAJILIWA YANGA

KIUNGO POLISI TANZANI- NIYONZIMA AMENIIBA NAFASI YANGU YA KUSAJILIWA YANGA

Habari za Yanga

KIUNGO wa Polisi Tanzania, Baraka Majogoro amesema kuwa kama asingekuwa Haruna Niyonzima kurejeshwa katika kikosi cha Yanga basi yeye angekuwa mmoja wa wachezaji wa timu hiyo ambayo ilikuwa ikimuhitaji.

 Niyonzima alisajiliwa na Yanga katika usajili wa dirisha dogo la usajili mwezi Januari akitokea katika timu ya AS Kigali ya Rwanda aliyojiunga akitokea Simba.Akizungumza na Championi Jumamosi, Majogoro alisema kuwa uongozi wa Yanga wakati wanatafuta mchezaji katika eneo la kiungo walimuhitaji yeye lakini baada ya kukamilisha usajili wa Niyonzima ghafl a walisitisha mazungumzo ya yeye kusajiliwa.

 “Viongozi wa Yanga walikuwa kwenye mazungumzo mazuri kabisa juu ya kunisajili lakini baada ya kukamilisha usajili wa kiungo Haruna Niyonzima waliachana na mimi maana walikuwa kimya sana siyo kama ambavyo walikuwa wakinisumbua kabla ya kumpata Niyonzima.

 “Nadhani kwa kuwa tulikuwa tunacheza wote sehemu moja ya kiungo ndiyo maana waliona waachane na mimi, haikuwa na jinsi kwani niliendelea kucheza kwa kiwango kizuri katika timu yangu ya Polisi Tanzania,” alisema kiungo huyo.

SOMA NA HII  MASHABIKI UINGEREZA KUPEWA RUKSA YA KUINGIA UWANJANI