Home Uncategorized MASHABIKI UINGEREZA KUPEWA RUKSA YA KUINGIA UWANJANI

MASHABIKI UINGEREZA KUPEWA RUKSA YA KUINGIA UWANJANI


 HUENDA mashabiki wa soka nchini Uingereza wanaweza kurejea tena viwanjani hivi karibuni, baada ya ombi la mashabiki kupata saini nyingi kutoka kwenye Bunge la Uingereza ambalo limepanga kuijadili taarifa hiyo Novemba 9, mwaka huu.

 

Tangu Machi, Serikali ilipiga marufuku mashabiki kuingia viwanjani kutokana na ugonjwa wa Corona, hivyo hatua hiyo endapo itafikiwa ni nafuu kwa vilabu vingi ambavyo vinategemea zaidi mapato ya mlangoni kuendesha klabu zao.

 

Licha ya kuchezwa bila ya mashabiki, ligi hiyo imeendelea licha ya ukweli kuwa  imepungua msisimko na ladha, ambapo mpaka sasa zimechezwa raundi nne.  


Timu ya  Everton inaongoza msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 12 wakishinda mechi zote  nne walizoshuka dimbani.

SOMA NA HII  NYOTA HUYU SIMBA ATAJWA KUBEBA MIKOBA YA BOCCO KWENDA POLOKWANE