Home Habari za michezo YANGA WAENDELEA KUWABAKISHA MASTAA WAO…LEO ZAMU YA ZAWADI MAUYA…ASAINI MKATABA MPYA WA...

YANGA WAENDELEA KUWABAKISHA MASTAA WAO…LEO ZAMU YA ZAWADI MAUYA…ASAINI MKATABA MPYA WA MAMILIONI YA PESA…

 


Kiungo Mkata Umeme wa Yanga, Zawadi Mauya ameongeza kandarasi ya kuendelea kuitumikia Klabu ya Yanga.

Taarifa iliyotolewa kwenye mitandao rasmi ya Klabu ya Yanga, haijaweka wazi Thamani wala muda wa Mkataba wa Kiungo huyo.

Zawadi alijiunga na Yanga mwaka 2020 akitokea Kagera Sugar yenye maskani yake Mkoani Kagera.

Pamoja na kiwango chake, Zawadi atakumbukwa na mashabiki wengi wa Yanga, ambapo alifanikisha kuipa ushindi muhimu timu yake katika mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya watani zao Simba SC.

Hivi karibuni, Yanga walianza kuwaongezea mikataba mastaa wao ambao walikuwa wanamaliza muda wa mikataba yao ya kuendelea kucheza kwa msimu huu.

Miongoni mwa mastaa ambao tayari wameshasaini mikataba mipya na kutangazwa ni pamoja na Kibwana Shomary, Bakari Nondo Mwamnyeto na leo hii ni Zawadi Mauya.

.

SOMA NA HII  BAADA YA WAARABU KUAMRIWA KUMLIPA FIDIA YA BIL1.6 ..MSUVA AWAPA SHARTI HILI GUMU...WAKIZINGUA FIFA INAWACHORA...