Home CAF KUELEKEA MECHI YA CAF…WASAUZI WAAMUA KUJA KIMACHALE MACHALE…SIMBA WANASA MIKANDA YAO YOTE…

KUELEKEA MECHI YA CAF…WASAUZI WAAMUA KUJA KIMACHALE MACHALE…SIMBA WANASA MIKANDA YAO YOTE…


WAKATI Simba wakijipanga, wageni wao Orlando Pirates nao wamejiwekea tahadhari kubwa wakisema wanatambua wanatakiwa kuwa makini na dakika 90 hizo za kwanza ugenini.

Kocha wa timu hiyo, Fadlu Davids alisema jana Simba ni timu ngumu hasa wanapokuwa nyumbani na wanatakiwa kujiandaa sawasawa kabla ya mchezo huo.

Davids aliongeza safu ya ushambuliaji ya Simba inaundwa na washambuliaji wenye kasi na tayari wameshaanza kufanyia kazi ubora huo.

“Tunakwenda kukutana na timu nzuri, timu inapofuzu hatua hii ni lazima uipe heshima ya ubora na wako (Simba) vizuri sana wanapocheza nyumbani,” alisema Davids.

“Simba wana washambuliaji wenye kasi. Hatutakiwi kufanya makosa mengi hatarishi, tumeshaanza kujipanga kabla ya kuanza safari.”

Simba ipo kambini ikijiandaa na mechi kubwa ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Orlando Pirates na tayari kocha wa wekundu hao, Pablo Franco amenasa mikanda mitatu ya Wasauz hao.

Taarifa kutoka ndani ya Simba ni kwamba mabosi wa juu wa klabu hiyo wamefanikiwa kunasa mechi tatu za Orlando walizocheza hatua ya makundi.

Mechi ambazo Simba imezipata ni tatu na kati ya hizo mbili ni zile ambazo Pirates imecheza dhidi ya JS Soura ya Algeria na Al Ittihad ya Libya na mchezo mmoja wa ligi.

Tayari mikanda hiyo imeshashuka kwenye benchi la ufundi la Simba na tayari watalaam wa kuchambua ubora wameshaanza kuzifanyia kazi.

SOMA NA HII  FAHAMU SIRI HII NZITO...ILIYOJIFICHA KWENYE MAFANIKIO YA YANGA...TIMU ILIKUWA HAINA MWENYEWE