Home Habari za Yanga FAHAMU SIRI HII NZITO…ILIYOJIFICHA KWENYE MAFANIKIO YA YANGA…TIMU ILIKUWA HAINA MWENYEWE

FAHAMU SIRI HII NZITO…ILIYOJIFICHA KWENYE MAFANIKIO YA YANGA…TIMU ILIKUWA HAINA MWENYEWE

Yanga kufanya vizuri ndani na nje ya nchi hakutokei kama bahati, ni mipango, uwekezaji, umoja na utulivu walionao kwa sasa kama klabu.

Kwa sasa Yanga wameungana kuliko wakati wowote ule, husikii vurugu zozote nje ya uwanja.

Wakati GSM wanaingia Yanga, waliikuta klabu kama vile imetupwa! Watu wote wa karibu walikuwa wameikimbia, ikafika wakati Kocha Mwinyi Zahera anaratibu mpaka safari, hoteli n.k. Kwa kifupi Yanga ilikuwa haina mwenyewe.

GSM wakaichukua Yanga ambayo ilikuwa imetelekezwa, hiyo ilikuwa faida kubwa sana GSM kwakuwa hakukuwa na watu waliokuwa na mpango na klabu kwa wakati huo, wote walikuwa mbali.

Kwa hiyo GSM akaingia na kuanza mchakato wa kuitengeneza Yanga anayoitaka yeye bila kupata presha ya watu wa nje. Ikawa ni rahisi kwao kuwaunganisha watu na kutengeneza watu wengine wapya ambao wanaendana kimtazamo.

Kwenye taasisi yoyote lazima awepo mtu mmoja ambaye amebeba maono halafu watu wengine wanakuja kuyatekeleza hayo maono.

Kukiwa na watu wenye malengo tofauti lazima taasisi itayumba.

GSM walichofanya ni kuchukua watu ambao wanaweza kutekeleza maono yao na kukaa pamoja kutengeneza mipango na kuanza kuitekeleza.

Kitu cha kuvutia, GSM hawakuikumbatia Yanga na kujifungia nayo hata wale waliokimbia wakati wa kipindi kigumu wanarudi kwenye timu.

Sasa hivi Yanga wanazungumza lugha moja, husikii tena matatizo yale ya zamani Yanga Kampuni, Yanga Asili wala Yanga ya Wazee.

Hivyo vitu havipo, imebaki Yanga moja chini ya uongozi mmoja. Hiyo ndio Yanga tunayoiona inaendelea kufanikiwa kila kukicha.

SOMA NA HII  FIGISU ZATAWALA SOKA LA AFRIKA...TIMU YAFANYA MAZOEZI AIRPORT...YAZUILIWA KUTOKA UWANHANI