Home Habari za michezo KUHUSU DILI LA OKRAH KUTUA YANGA UKWELI WOTE HUU HAPA….ENG HERSI AINGILIA...

KUHUSU DILI LA OKRAH KUTUA YANGA UKWELI WOTE HUU HAPA….ENG HERSI AINGILIA KATI…

Tetesi za usajili Yanga

ALIYEKUWA kiungo mshambuliaji wa Simba, Augustine Okrah amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia kikosi cha Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga kioindi hiki cha usajili wa dirisha dogo.

Nyota huyo tayari ameshawasili nchini na kujiunga na timu hiyo na kuwepo kwenye msafara wa kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuondoka leo kuelekea visiwani Zanzibar kwa ajili ya michuano ya kombe la Mapinduzi.

Okrah utakuwepo katika mchezo wa kwanza wa michuano ya Mapinduzi ambapo watacheza kesho (Jumapili) dhidi ya Jamhuri ya Visiwani humu, katika Uwanja wa Amaan Complex.

Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema kifaa kipya ambaye ni mgeni mwenyeji alitakiwa kumtambulisha leo  lakini Rais wao,Hersi Said alitaka wakamtambulishe visiwani Zanzibar.

Amesema kwa hali hiyo nyota huyo (Okrah) atatambulishwa jumapili katika mchezo wa kwanza wa kombe la Mapinduzi ambapo watacheza dhidi ya Jamhuri.

“Huyu mchezaji ni mgeni lakini mwenyeji tunatarajia kumtambulisha katika mchezo wetu wa kwanza, utambulisho wake utafunika ile shoo ya msanii Diamond aliyoifanya pale uwanja wa Amaan.

Usajili ambao unaganya ni kulingana na mapendekezo ya kocha Gamondi (Miguel) kuhakikisha tunaimarisha kikosi chetu na kuwa imara,” amesema Kamwe.

Ameongeza kuwa timu inaondoka leo kuelekea visisani humu wakiwa na dhamila ya kutwaa taji la ubingwa la michuano hiyo, kwa kwenda kikosi cha wachezaji wote kasoro wale walioitwa katika majukumu ya timu ya Taifa.

“Safari hii tumejipanga vizuri kwenda visiwani Zanzibar kwemda kuchukuwa ubingwa wa michuano hiyo, kwa kuangalia timu nne zilivyocheza basi wasubiri kuona Yanga wanaingia kuwafundisha soka.

Tunaenda na mambo mawili mmoja kuwapa zawadi Rais wa kwa ujezi mzuri wa uwanja wa Amaan na nyingine mashabiki wa Yanga kuwapa zawadi ya kufungia mwaka,” amesema Kamwe.

Kuhusu Okrah amesema wanakuwa na tetesi nyingi sana hasa kipindi cha usajili lakini mashabiki wa Yanga wanatakiwa kuwa wavumilivu na kusubiri jumapili kumuona huyo Mgeni mwenyeji.

Mbali na Okrah, nyota wengine wanaotajwa kusajiliwa na Yanga ni Simon Msuva na mshambuliaji kutoka klabu ya Dynamo Dougla ya Cameron, Leonel Ateba.

SOMA NA HII  YANGA WAMKATAA MWAMUZI WA SIMBA SC