Home Habari za michezo WAKATI SUALA LA OKRAH LIKIVUMA…MGUNDA NAYE KAIBUKA NA HILI KUHUSU YANGA….

WAKATI SUALA LA OKRAH LIKIVUMA…MGUNDA NAYE KAIBUKA NA HILI KUHUSU YANGA….

Kocha Msaidizi Simba SC

KOCHA Mkuu wa Simba Queens, Juma Mgunda ameweka wazi sasa mipango na nguvu zao kuelekeza katika mechi ijayo ya watani wa jadi dhidi ya Yanga Princess, utakaochezwa Januari 3, 2024.

Simba iliibuka na ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Baobab Queens ikiwa ni mchezo wa raundi ya pili ya Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania, uliocheza uwanja wa Azam Complex, uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam .

Kocha Mgunda amesema wamemaliza mchezo na Baobab Queens salama na hakukuwa na majeraha makubwa sana na kuwapongeza wachezaji wake kuendelea kupata alama tatu muhimu.

Amesema pamoja na ushindi mnono wa mabao 5-2 dhidi ya Baobab Queens bado ameona mapungufu na kufanyia kazi mazoezini kuyaondoa yale mapumgufu na kuhakikisha wanaimarisha katika ubora wao.

“Kila mechi ilikuwa na mipango yake ya kutafuta pointi tatu muhimu lakini kuna mapungufu ikiwemo kuruhusu bao mbili, tunaenda kufanyia kazi makosa yetu hayo ya safu ya ulinzi lakini pia tulitengeneza nafasi na hatukuweza kutumia.

Hii ni Derby lazima tujipange vizuri, tunarudi kwenye uwanja wa mazoezi kwa lengo likiwa kuhakikisha tunapata pointi tatu kwenye kila mechi ili kufikia malengo yetu,” amesema Mgunda.

Nahodha wa Simba, Vivian Corazone amesema, ligi ngumu kila kitu imejiamdaa vizuri lakini kwao kila mechi ni fainali na wanapambana kusaka alama tatu katika kila mechi.

Amesema baada ya ushindi wa mabao 5-2 na Baobab Queens, nguvu zao wanazielekeza katika mechi ya Derby dhidi ya Yanga Princess kutafuta matokeo chanya kama ilivyo kwa mechi zilizopita.

“Ligi imekuwa ngumu na timu zote zimejiandaa vizuri na tunarudi uwanja wa mazoezi kujiwinda na mchezo wetu dhidi ya Yanga, lengo ikiwa ni kuchukuwa pointi zote tatu dhidi ya watani wetu,” amesema Vivian.

SOMA NA HII  SIMBA WAKOSA MDHAMINI TUZO ZA MCHEZAJI BORA WA MWEZI....

1 COMMENT