Home Habari za michezo KOCHA WA ASEC MIMOSAS AKUBALI KUWAACHIA YANGA KIFAA HIKI…WARABU WANATAMBUA JOTO LAKE…

KOCHA WA ASEC MIMOSAS AKUBALI KUWAACHIA YANGA KIFAA HIKI…WARABU WANATAMBUA JOTO LAKE…

Tetesi za usajili Yanga

KOCHA wa Asec Mimosas, Julien Chevalier amesema hana kizuizi kwa supastaa wake Karamoko Sankara kwenda Yanga, lakini litakuwa pigo kwa timu yake.

Yanga imekuwa ikitajwa kutaka saini ya mshambuliaji huyo ambaye kwa sasa ndiye kinara wa mabao kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa ameshatupia manne – moja zaidi ya Pacome Zouzoua wa Yanga.

Mshambuliaji huyo mwenye asili ya Ivory Coast amekuwa kwenye ubora wa juu na tetesi zimekuwa zikimhusisha zaidi na Yanga, ingawa haitaweza kumtumia kwenye Ligi ya Mabingwa msimu huu kwa kuwa ameshaitumikia Asec.

Julien ambaye timu yake imeshafuzu hatua ya robo fainali ikitokea Kundi B, ikiwa pamoja na Simba, Jwaneng Galaxy na Wydad Casablanca alisema kama ataondoka, basi watakuwa na kipindi kigumu hasa katika michuano ya kimataifa kwani ni mchezaji tegemeo ambaye bado anamhitaji.

Alisema licha ya kuwa katika nafasi nzuri bado wanahitaji ushindi ambao unaletwa na wachezaji wazuri kama mshambuliaji huyo, lakini uwezekano wa kuondoka unategemea na maamuzi ya uongozi wa klabu.

“Asec haizuii mchezaji kuondoka kama kuna timu itakuwa inamtaka, ila kama akiondoka kwa hatua tuliyopo basi tutapoteza mchezaji muhimu ambaye amekuwa kwenye kiwango bora msimu huu.

“Sisi tuna utaratibu wa kuwaruhusu wachezaji kuondoka kama wanakwenda kupata maslahi mazuri zaidi na huyu pia tunaweza kumruhusu, lakini nilitamani kuona anaondoka mwishoni mwa msimu siyo sasa.

“Timu ndiyo huwa inapata wakati mgumu mchezaji mkubwa akiondoka, mfano Aziz Ki na Pacome Zouzoua walikuwa bora lakini Yanga ilipowahitaji basi waliondoka na huyu itakuwa hivyo hivyo,” alisema Julien.

Asec ambayo ilitoka sare ya bao 1-1 na Simba kwenye Uwanja wa Mkapa zitakutana tena Februari 23 2024 nchini Ghana, ikiwa ni mchezo wa marudiano wa kufuzu hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika ambao utaamua hatima ya timu hiyo ya Msimbazi kufuzu au kutofuzu hatua ya robo fainali.

Asec imekuwa moja ya timu za Afrika ambayo inawasajili wachezaji wa kiwango cha chini cha fedha na baadaye inawauza kwa fedha nyingi bila kujali ni kipindi gani au mchezaji ana umuhimu gani kwenye timu kwa wakati huo.

SOMA NA HII  STAA MPYA YANGA AWEKA REKODI YA KIBABE TZ...KUMBE ALIKUWA MCHEZA DANSA...