Home Uncategorized MTUPIAJI WA YANGA PRINCESS ASAINI SIMBA QUEENS

MTUPIAJI WA YANGA PRINCESS ASAINI SIMBA QUEENS

 

SHELDA Boniphace mshambuliaji wa  Yanga Princess msimu wa 2019/21 ameibukia ndani ya watani zao wa jadi Simba Quuens.

Akiwa ndani ya Yanga Princess kwa msimu wa 2019/20 alitupia jumla ya mabao 11 ndani ya Ligi ya Wanawake jambo lililowafanya Simba wakavutiwa na uwezo wake.

Kocha Mkuu Simba Queens,  Mussa Mgosi amesema kuwa malengo makubwa ya timu hiyo ni kuendelea kuwa bora na kuleta ushindani Afrika Mashariki na Kati.

“Tupo imara katika maboresho yetu na kikosi chetu kimeonekana kwa msimu uliopita ambapo tumeweza kutwaa ubingwa tukiwa na mechi mkononi, bado tunahitaji kuendelea kutwaa mataji hivyo tunaboresha kikosi ili kuwa imara zaidi,” amesema.

SOMA NA HII  STARS YABANWA MBAVU NA SUDAN YACHAPWA BAO 1-0