Home Uncategorized KIFAA KINGINE AFCON KUSAINI YANGA

KIFAA KINGINE AFCON KUSAINI YANGA


Jina la mshambuliaji Rashid Mandawa lipo kwenye orodha ya mastaa wanaotakiwa pale Yanga.

Kama ulikuwa unajua kuwa Yanga wamemaliza kufanya usajlli wa washambuliaji basi umejidanganya kwani wapo kwenye mpango wa kumsainisha Mandawa ambaye yupo kwenye michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) inayoendelea
nchini Misri.

Mshambuliaji huyo ambaye anaitumikia BDF XI ya Botswana, inadaiwa yuko kwenye mipango ya Kocha Mwinyi Zahera hivyo ni kati ya mastaa wazawa ambao wanatakiwa Yanga.

“Mandawa yupo kwenye ile orodha ya mwalimu ambapo alisema kuwa tumsainishe kwa kuwa ni mzawa kwani anaweza kutuongezea kitu. Hata hivyo hajatubana zaidi alisema tumsajili kama fedha itapatikana,” kilisema chanzo.

SOMA NA HII  MROMANIA WA AZAM FC KUANZA SAFARI YAKE NA GARI