Home Uncategorized MAYANJA KUIBEBA KMC KAGAME

MAYANJA KUIBEBA KMC KAGAME


UONGOZI wa timu ya KMC, jana ulimtambulisha Mganda, Jackson Mayanja kuwa ndiye kocha wao mkuu ambaye ataanza kazi kwenye michuano ya Kombe la Kagame.

KMC iliondokewa na kocha wao, Ettiene Ndayiragije ambaye ametimkia Azam FC na sasa imemshusha Mayanja ambaye amewahi kuzifundisha Klabu za Simba, Coastal Union na Kagera Sugar.

Mayanja amepewa mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza endapo atatizimiza malengo. Akizungumza na Spoti Xtra, Mayanja alisema kuwa, ana uzoefu na Ligi Kuu ya Tanzania, hivyo haoni tabu kurejea Tanzania na ataanza kuandaa kikosi kwenye michuano ya Kombe la Kagame ambayo itaanza Julai, mwaka huu.

“Natambua kwamba KMC ni timu kubwa na inashiriki michuano ya kimataifa ambayo ni Kombe la Shirikisho, hivyo nitaanza kuandaa kikosi cha maangamizi kupitia michuano ya Kagame ambayo tutashiriki.

“Ushindani kimataifa ni mkubwa, hilo nalitambua ila ubora wa timu pamoja na mbinu nitakazowapa wachezaji wangu nitakaowapata itasaidia kuongeza uwezo na matokeo chanya,” alisema Mayanja.

SOMA NA HII  10 BORA NDANI YA LIGI KUU BARA