Home Habari za michezo ULE MPANGO WA BWALYA KUTAKIWA AFRIKA KUSINI UKO HIVI….AMAZULU FC WAANZA KUTUPA...

ULE MPANGO WA BWALYA KUTAKIWA AFRIKA KUSINI UKO HIVI….AMAZULU FC WAANZA KUTUPA ‘NDOANO BAHARINI…’


Wakati Tetesi zikieleza kuwa huenda Simba SC wakamuacha Rally Bwalya mwishoni mwa msimu huu, Kiungo huyo anatajwa kuwindwa na klabu ya Amazulu FC inayoshiriki Ligi Kuu Afrika Kusini.

Taarifa zilizoripotiwa na Soccer Bullet zinasema Kiungo Rally Bwalya yupo kwenye Rada za Klabu ya Amazulu FC ambayo imemfuatilia na kuridhishwa na uwezo wake.

Bwalya ni moja ya wachezaji waliofanya vema sana ndani ya kikosi cha Simba SC, baada ya kuwa sehemu ya timu iliyofika Robi Fainali Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika, huku ikitwaa taji la Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho β€˜ASFC’ msimu uliopita.

Mwenyekiti wa Amazulu Sandle Zungu kwa sasa anatumia nguvu Kubwa sana kusuka kikosi cha ushindani ili aweze kuvunja utawala wa Mamelodi Sundowns ndani ya Premier League Soccer (PSL) ambao wametawala kwa miaka mingi hivi sasa.

Amazulu ni moja ya Klabu TAJIRI pale Africa Kusini pia ikiwa na wadhamini Lukuki kwa sasa wameamua kutumia pesa za Mwana mfalme Ilikuwa timu kipenzi ya King Zwellatin hayupo Duniani kwa sasa.

SOMA NA HII  MORRISON AIBUKA UPYA YANGA...ALLY KAMWE ATOA KAULI YA KLABU...NKANE NAYE NDANI...