Home Habari za michezo ISHU YA MORRISON KUZUIWA KUINGIA SAUZI..MASHABIKI WA SIMBA SAUZI WAIBUKA NA HILI..WATOA...

ISHU YA MORRISON KUZUIWA KUINGIA SAUZI..MASHABIKI WA SIMBA SAUZI WAIBUKA NA HILI..WATOA ONYO…


Mashabiki wa Simba wanaoishi Afrika Kusini wameanza kujipanga mapema kuipokea timu hiyo itakapoenda kurudiana na Orlando Pirates katika mechi ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Timu hizo zitakutana kwa mara ya kwanza katika michuano ya CAF Aprili 17 kabla ya kurudiana wiki moja baadae Sauzi na tayari mashabiki wa Msimbazi waliopo huko wameanika walivyojipanga.

Akizungumza Mtanzania anayeishi Saudi, Abdallah Mabange mnazi wa Simba alisema droo hiyo wameipokea vizuri kabisa na wako tayari kuwapokea wekundu hao watakapokwenda huko.

Alisema wao hawana shughuli ndogo watakuwa na amsha amsha nyingi kuanzia nje hadi uwanjani kwa kuwa hivi sasa mashabiki wanaruhusiwa kuingia.

“Orlando yenyewe inaihofia Simba, chama letu lisiogope wenyeji tupo wa kutosha huku, mwaka jana tulishindwa kuwasapoti zaidi kutokana na janga la Uviko-19 kwani kulikuwa na katazo,” alisema Mabange.

Alisema kwa jinsi winga Bernard Morrison alivyokiwasha katika mechi iliyoivusha timu kwa ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya a USGN alikuwa ni muhimu katika mchezo wa Sauzi, ila haruhusiwi kuingia huko.

“Yaani huku Morrison ni wanted kweli, naamini wachezaji wengine watatuwakilisha ila yeye apambane katika mchezo wa nyumbani kuhakikisha tunashinda mabao mengi, tukirudi hapa tunakamilisha tu mahesabu,” alisema Mabange.

Naye Greyson Ezekiel ‘Jujuman’, kaka wa nyota wa filamu nchini, Aunty Ezekiel alisema, japo kwa sasa yuko nchini Eswatini kwenye mambo yake ila hadi mnyama anaenda atakuwa amerejea nchini humo.

“Mimi Simba kweli damu, baba yangu tu aliwahi kucheza Simba, sibahatishi, hawa Orlando hawatutishi hata kidogo nina imani kubwa na wachezaji wangu pamoja na uongozi madhubuti,” alisema.

Simba inakutana na timu ya Sauzi kwa mara ya pili mfululizo baada ya awali msimu uliopita iling’olewa na Kaizer Chiefs kwa ushindi wa jumla ya mabao 4-3, ikilala ugenini 4-0 kabla ya kuzinduka nyumbani kwa ushindi wa 3-0.

SOMA NA HII  PAMOJA NA KIPOGO CHA JANA...SIMBA WAPELEKA AKILI UGANDA NA GUINEA...