Home Habari za michezo SIKU MOJA BAADA YA YANGA KUFUNGWA …FEI TOTO AIBUKA NA JIPYA HILI...

SIKU MOJA BAADA YA YANGA KUFUNGWA …FEI TOTO AIBUKA NA JIPYA HILI TENA…”NATAMANI KURUDI”…

Tetesi za Usajili Yanga

Baada ya juhudi za Mchezaji Feisal Salum “Fei Toto” kugonga mwamba mara mbili TFF kwa kushindwa kukubaliwa ombi lake la kuvunja mkataba na Yanga na Mchezaji huyu juzi kutangaza kuomba msaada wa pesa kwa Watanzania ili aweze kwenda kwenye Mahakama ya usuluhishi wa kimichezo (CAS), leo tena amekazia ombi lake na kuomba Watu wamchangie ili arudi uwanjani.

Feisal ameandika yafuatayo katika taarifa yake; “Ndugu zangu Watanzania, natamani kurdi uwanjani na kuendelea kuwafurahisha wapenda soka, nimebakisha hatua chache, nisaidieni niweze kukamilisha nia yangu ya kwenda CAS na kupata haki ya kurudi tena uwanjani”

“Nimekumbuka nyakati bora, nimekumbuka kupiga mashuti yangu ya mbali, nimekumbuka kufurahia na Mashabiki wa soka, Fei Toto ni mmoja tu, msaidie arudi uwanjani kwa haki inayotaka kudhulumiwa”

“Unaweza kulipia kwa lipa namba (5406394 FEISAL SALUM) hapo pichani au kwa namba hii ya simu kwa kwa Tigo Pesa 067 912 8899 FEISAL SALUM ABDALLAH, aidha natoa pole kwa kifo cha Shabiki wa Soka na majeruhi katika kadhia ya Jana, ALLAH ATAWAPONYA INSHALLAHl”

Fei toto ameanziha kampeni ya kuomba achangiwe zaidi ya mili 56 za kwenda kulipia gharama ya kufungua kesi CAS baada ya kuona mamlaka za soka hapa nchini hazijamtendea haki katika dai lake la msingi la kutaka kuvunja mkataba na Yanga.

Mwanzoni mwaka huu, Fei Toto aligoma kuichezea Yanga kwa kile alichodai kuwa maslahi anayolipwa ni kidogo tofauti na kazi anayoifanya.

Hatua hiyo ilimepelekea kutaka kuvunja mkataba na klabu hiyo ambayo ilimsjaili misimu minne nyuma akitokea iliyokuwa klabu ya Sindiga United.

Katika madai yake hayo kwa Yanga, Fei toto alisema kuwa kwa sasa kiwango chake ni kikubwa mno kiasi ambacho hastahili tena kulipwa mshahara wa milioni 4 huku wachezaji wa Kimataifa wenye kiwango sawa na chake wakilipwa zaidi ya Milioni 10.

Mvutano huo ulimfanya agomee kushiriki mazoezi na mechi za timu hiyo, huku akishinikiza mkataba wake uvunjwe atafute maslahi sehemu nyingine.

Katika kushindilia matakwa yake hayo, Fei Toto alilipa kiasi cha Milioni 100 kama gharama za kuvunja mkataba wake na Yanga kwa mujibu wa makubaliano ya pande mbili.

Yanga nao kwa upande wake baada ya kuona hawako tayari kumuachia nyota wao, waliamua kutaka kukaa naye chini na kuzungumza huku wakimwahidi kumlipa kiwango sawa na mastaa wa klabu hiyo kiutoka nnje ya Tanzania.

SOMA NA HII  AKILI YA SIMBA SASA NI KWA COASTAL UNION, MSUTUPANGIE KIPA LANGONI