Home Habari za michezo M’BAYA WA SIMBA MIKONONI MWA YANGA….MAMBO YAPELEKWA KIMYA KIMYA AISEE..

M’BAYA WA SIMBA MIKONONI MWA YANGA….MAMBO YAPELEKWA KIMYA KIMYA AISEE..

Habari za SImba SC

Mwamba aliyepeleka kilio kwa Simba SC, Prince Dube, ameingia mikononi mwa Yanga kwa kuwa kwenye kipengele kimoja cha kuwania tuzo.

Dube aliwatungua Simba kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports likiwa la ushindi, ilikuwa Mei 7, 2023 ubao wa Uwanja wa Nangwanda Sijaona uliposoma Azam FC 2-1 Simba.

Bao la ushindi kwa Azam FC lilifungwa na Dube dakika ya 73 na kuwafungashia virago Simba kwenye mashindano hayo.

Katika orodha iliyotolewa na Kamati ya Tuzo za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), wachezaji watano wameteuliwa kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports, (ASFC).

Dube na Abdul Suleiman ‘Sopu’ wote wa Azam FC, Bakari Mwamnyeto, Fiston Mayele na Clement Mzize wote kutoka Yanga.

Mastaa wote hao watakutana kwenye mchezo wa fainali utakaochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, ambapo bingwa mtetezi ni Yanga.

SOMA NA HII  UBORA WA MIQUISONE NA KINACHOENDELEA KWA MASHABIKI