LEO Septemba 7 Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea ambapo timu zitakuwa kwenye msako wa pointi tatu muhimu.
Simba itakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya KMC kwenye mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.
Ni Seleman Matola atakiongoza kikosi hicho ambacho kwenye mchezo wa leo baada ya Zoran Maki kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba wake.
Pointi sita wanazo Simba wakiwa nafasi ya pili na KMC ina pointi moja baada ya kucheza mechi mbili.
Mtibwa Sugar watawakaribisha Ihefu FC kwenye mchezo wa ligi unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Manungu.