Home Yanga SC GSM WAFUNGUKA KUHUSU TAARIFA ZA KAZE KUFUKUZWA YANGA

GSM WAFUNGUKA KUHUSU TAARIFA ZA KAZE KUFUKUZWA YANGA


MAKAMU Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Injinia Hersi Said amesema kuwa wana mipango mirefu na Kocha Mkuu wa timu hiyo Cedric Kaze hivyo bado yupo ndani ya kikosi hicho.

Hivi karibuni kumekuwa na presha kubwa kwa Kaze kutajwa kuwa amepewa mechi kadhaa ili aweze kuchimbishwa kutokana na kuwa na mwendo ambao hauridhishi.

Taarifa zimekuwa zikieleza kwamba mabosi wa Yanga wapo kwenye mpango wa kumfuta kazi kocha huyo ili waweze kuleta kocha mpya.

Kwenye mechi za mzunguko wa pili baada ya kuongoza kwenye mechi nne ambapo amekuwa na mwendo wa kusuasua.

Alianza kwa sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Nelson Mandela, sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Mbeya City na sare ya kufungana mabao 3-3 dhidi ya Kagera Sugar.

Ameshinda bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar na bao 1-0 dhidi ya Ken Gold kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya 32 bora na timu hiyo imetinga hatua ya 16 bora.

Injinia ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya GSM ambao ni wadhami wa Klabu ya Yanga, amesema:”Kaze yupo ndani ya Yanga kwa muda mrefu kwa kuwa ni mwalimu ambaye tumemwamini na hakuna ambaye anafikiria kuachana naye.

“Kuna timu nyingi duniani ambazo zimekuwa zikipata matokeo mabovu ikiwa ni pamoja na ile ya Liverpool ambayo inanonolewa na Kocha Mkuu, Jurgen Klopp.

“Hivyo kupata matokeo mabovu haina maana kwamba Klopp ni mbovu, na timu yetu haijapata matokeo mabaya na haina matokeo mabovu kwa kuwa bado haijapoteza mechi yoyote ya ushindani,” amesema.

Kwa sasa timu ipo Tanga na kesho ina kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Mzunguko wa kwanza Yanga ilishinda mabao 3-0 hivyo kesho kila timu itakuwa inahitaji kuweka rekodi yake, Yanga kulinda na Coastal Union kutibua.

SOMA NA HII  NABI ATANGAZA KIAMA YANGA...ATOA MSIMAMO MKALI KUHUSU DAKIKA 270