Home Simba SC ONYANGO:KELELE ZIMEPUNGUA KWA WALIOKUWA WANANIPONDA BAADA YA KUWAFUNGA YANGA

ONYANGO:KELELE ZIMEPUNGUA KWA WALIOKUWA WANANIPONDA BAADA YA KUWAFUNGA YANGA

 

JOASH Onyango, beki chaguo namba moja ndani ya Klabu ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes amesema kuwa bao lake la kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara liliwapunguzia kelele wapinzani waliokuwa wakimponda.

Onyango alipachika bao hilo Uwanja wa Mkapa kwenye dabi yake ya kwanza wakati Yanga ikilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 ilikuwa zama za Sven Vandenbroeck. 

Bao la Yanga lilipachikwa kipindi cha Kwanza na Michael Sarpong kwa mkwaju wa penalti baada ya mwamuzi wa kati kutafsri kwamba Onyango alimchezea rafu ndani ya 18 mzee wa spidi Tuisila Kisinda. 

Bao hilo lilidumu mpaka kipindi cha pili lilisawazishwa na Onyango mwenyewe dakika za lala salama kwa kichwa baada ya beki wa Yanga, Bakari Mwamnyeto kuokoa hatari ya Shomari Kapombe na kusababisha iwe kona.

Kona hiyo ilipigwa na Luis Miquissone ikakutana na kichwa cha Onyango ambaye alimtungua kipa namba moja Metacha Mnata na kufanya ubao usome 1-1.

Beki huyo amesema:”Bao langu la Kwanza mbele ya Yanga nilifurahi mno kwa kuwa nilikuwa naskia kwamba wanasema nimefanya makosa, sasa baada ya kufunga nikawa nimesawazisha makosa yangu ila haikuwa dhamira yangu kukosea,”.

Simba leo Machi 3 inatarajiwa kuanza safari kuelekea Sudan mwa ajili ya mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Merrikh unaotarajiwa kuchezwa Machi 6.

SOMA NA HII  MRITHI WA MIKOBA YA SVEN NI HUYU HAPA