Home Habari za michezo BREAKING NEWS: SIMBA SC YAANZA NA MAGORI & NKWAMBI

BREAKING NEWS: SIMBA SC YAANZA NA MAGORI & NKWAMBI

HABARI ZA SIMBA

Mnyama Simba SC ameanza kuonesha makucha yake baada ya kukaa kinyonge kwa misimu mitatu mtawalia bila ubingwa wa Ligi Kuu Bara, ambapo kwa miaka yote hiyo Yanga SC wametawala sana ndani ya uwanja na nje ya uwanja.

Uongozi wa Simba umeonesha nia thabiti kabisa ya kufanya makubwa kwenye usajili msimu huu, kwa kufanya umafia wa kuwarejesha kwenye kamati viongozi wao wa zamani ambao walifanya makubwa sana miaka hiyo.

Soka la Bongo limepata mafile na habari za ndani kutoka Uongozi wa Simba kwamba, Mwenyekiti wa Zamani wa klabu ya Simba SC Swedy Nkwambi pamoja na “master plan” Crescentius Magori, ambaye aliwahi kuwa CEO wa klabu hiyo wamerudishwa na kupatiwa majukumu mapya.

Habari zinaeleza kwamba, Magori na Nkwambi kwa pamoja wamepatiwa majukumu ya kuongoza kamati ya usajili ya Mnyama Simba SC, hii ni kutokana na sajili mbovu zilizokuwa zikifanyika kwa hivi karibuni.

Simba SC ilikosa watu sahihi wa kusimamia usajili na hili limeonekana kwenye, sajili nyingi zilizofanywa na viongozi hao.

SAJILI ZILIZOFELI SIMBA SC MIAKA YA KARIBUNI.

Yusuf Mhilu, Peter Banda, Ismail Sawadogo, Duncan Nyoni, Junior Lokosa, Jeremia Kisubi, Habib Haji Kiyombo, Par Omar Jobe, Dejan Gejovic, na mastaa wengine kibao.

Magori ni mshauri mkubwa wa Rais wa Heshima wa Simba na muwekezaji wa klabu hiyo, na hivi karibuni baada ya kusuasua kwa timu hiyo, aliibuka na kusema kwamba ameongea na Mohammed Dewji MO, na aliahidi kwamba hawezi kuiacha Simba na hatokuja kuiacha Simba.

” MO yupo tayari kushirikiana na Uongozi na kurudisha makali ya Simba na kuijenga Simba Imara”

Itakumbukwa kwamba enzi wa uongozi wa Magori ndani ya Simba SC, ndiye aliyehusika kufanya sajili za maana kabisa kwa kumleta Clatous Chama akishirikiana na Hayati Hans Pope, pia usajili wa Rally Bwalya Maestro, sajili zote hizi zilifanya poa sana.

Kwahiyo usajili wa msimu wa dirisha hili utasimamiwa na Magori pamoja na swahiba wake, Swedy Nkwambi. Wanasimba kaeni mkao wa kula.

SOMA NA HII  SIMBA YAKIMBILIA CAF MECHI NA WYDAD...VAR ITATUMIKA...MANULA,KANOUTE OUT