Home Habari za michezo SIMBA SC KUSHUSHA WINGA… ANATOKA DR CONGO.. NI FUNDI HASWA

SIMBA SC KUSHUSHA WINGA… ANATOKA DR CONGO.. NI FUNDI HASWA

KLABU ya Simba wapo kwenye mazungumzo na mshambuliaji kutoka klabu ya AS Vita, Elie Mpanzu, ili  kupata huduma yake.

Simba  ipo kwenye mchakato wa kuboresha timu kwa kufanya usajili mzuri kwa ajili kukiimarisha kikosi, huku ikitarajia  kucheza kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao, baada ya kupoteza nafasi ya kwenda ligi ya Mabingwa Afrika.

Taarifa zilizopatikana kutoka chanzo, kinadai mazungumzo yalianza kufanyika mapema na mambo yakiwa mazuri utakuwa ni usajili wa kwanza kwa wachezaji wapya ambao wanasajiliwa kwa msimu ujao wa mashindano.

Imeelezwa kuwa viongozi wameanza kusuka kikosi cha timu hiyo kwa msimu ujao kwa kuangalia katika nafasi hasa ushambuliaji ilikuwa tatizo ndani ya Simba baada ya kuondoka kwa Mosse Phiri na Jean Baleke.

“Baada ya kuondoka wachezaji hao, wakaletewa Pa Omar Jobe na Fred Michael lakini hawakuonyesha kile kilichotarajiwa na wanasimba, watu waliopewa jukumu la usajili wameanza kuingia sokoni na Mpanzu ni miongoni mwa nyota ambao wako kwenye mazungumzo,” kilisema chanzo hicho.

Meneja wa Idara ya habari na Mwasiliano ya Simba, Ahmed Ally amesema mipango yao ni kuboresha kikosi suala la nani anasajiliwa hilo lipo kwa watu maalum wanaohusika na masuala ya usajili.

“Ni kweli maboresha yatafanyika lakini suala la usajili ni siri kwa sasa kwa sababu, tunahitaji kuleta vifaa bora kulingana na mapendekezo ya benchi la ufundi na mahitaji ya timu yetu kwa msimu ujao wa mashindano ikiwemo kombe la Shirikisho la Afrikia,” amesema Meneja huyo.

SOMA NA HII  HAJI MANARA AGOMEA ISHU YA KUOMBA MSAMAHA KWA YANGA