Home Habari za Simba Leo KUMNUNUA FEI TOTO NI BIL 1.3…SIMBA, YANGA ZAPIGANA VIKUMBO

KUMNUNUA FEI TOTO NI BIL 1.3…SIMBA, YANGA ZAPIGANA VIKUMBO

habari za simba- Fei Toto

SIKU za hivi karibuni kumeibuka taarifa za mchezaji wa Azam FC Feisal Salum Fei Toto, kuhitajika na vilabu vikubwa ndani na nje ya nchi ikiwemo Mamelod Sundowns.

Kwa vila vya ndani ni Simba na Yanga wote wanaivizia tena saini ya Fei Toto, kwa upande wa Yanga ni wanafikiria namna ya kumrudisha tena mchezaji huyo.

MKATABA WA FEI TOTO UKO HIVI.

Mkataba wa Fei Toto na Azam una kipengele cha kuvunjwa kwa $500,000 (Tsh 1,362,220,000 ) ndani ya miaka miwili ya kwanza.

Lakini ifikapo mwishoni mwa msimu huu thamani ya mkataba huo itapungua hadi $250,000 (tsh 681,110,000).

Hivyo timing ya vilabu vingi iko pale mwishoni mwa msimu ambapo tsh 600m itatosha kuvunja mkataba wa Fei.

Lakini pia Azam wanapambana kumuongezea mkataba mpya ili waendelee kuwa na power juu yake.

SOMA NA HII  KUTOKA SUDAN: WENYEJI WA SIMBA WAMKUNG'UTA MTU GOLI 5 BILA...ZORAN NA JESHI LAKE KUANZA KAZI KESHO...

1 COMMENT

  1. […] wa kimataifa wa Tanzania Feisal Salum Abdallah (Fei Toto) amepiga chini ofa ya pili kutoka Azam ambayo ilimtaka kuongeza mkataba […]

Comments are closed.