Home Habari za michezo SIMBA YAKIMBILIA CAF MECHI NA WYDAD…VAR ITATUMIKA…MANULA,KANOUTE OUT

SIMBA YAKIMBILIA CAF MECHI NA WYDAD…VAR ITATUMIKA…MANULA,KANOUTE OUT

Habari za Simba SC

Uongozi wa Simba umeweka wazi kuwa malengo makubwa kuelekea mchezo wao dhidi ya Wydad Casablanca kutoka Morocco ni kupata ushindi utakaowafanya wavunje mwiko wa kugotea katika hatua ya robo fainali katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Jumamosi hii Simba kwenye Uwanja wa Mkapa wataakaribisha Waydad saa 10:00 jioni kwa ajili ya kucheza nao mchezo wa kwanza wa michuano hiyo kabla ya kwenda kurudiana nao Aprili 28, huko Morocco.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Ahmed Ally ambaye ni Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba alisema wanawaheshimu wapinzani wao na watafanya maandalizi maalumu juu yao kuelekea katika mchezo huo muhimu.

“Mechi hii dhidi ya Wydad tumeomba iwe saa 10:00 jioni CAF ili kila Mwanasimba aje kumuona mnyama akifanya yake.

“Kikosi kimeingia kambini leo (jana) baada ya kutoka kumnyoa mtani (Yanga) Uwanja wa Mkapa, wachezaji walipewa mapumziko ya siku moja na sasa wote wameingia kambini na tutaanza mazoezi rasmi kwa ajili ya mchezo wetu.

“Sadio Kanoute hajaonekana kwenye mechi dhidi ya Raja Casablanca pia dhidi ya Ihefu alikuwa nje kutokana na kusumbuliwa na nyonga tayari amepata matibabu madaktari watamuangalia kama ataweza kuanza mazoezi na wengine.

“Aishi Manula yeye anapatiwa matibabu na ripoti ya madaktari itaamua kama anaweza kufanyiwa upasuaji ama anaweza kuanza mazoezi.

“Mechi yetu dhidi ya Wydad hatua ya robo fainali itaamuliwa na VAR na waamuzi wanatarajiwa kuwasili leo (jana) wapinzani wetu wanatarajiwa kuwasili kesho (leo) wakiwa na msafara wa watu 50, wakiwa na ndege yao binafsi.

“Mwamuzi wa kati atakuwa anatokea Senegal pia waamuzi wote hawa wote wanawasili kesho (leo) pamoja na waamuzi wa VAR.

“Hii ni mechi kubwa kwa kuwa Wydad Casablanca inatetea ubingwa Afrika inakwenda kuangalia namna gani Simba itafanya je, itarudia historia ya 2003 dhidi ya Zamalek tulipomfanyia kitu kibaya, haitaamini macho yake, dhamira yetu ni kuvunja mwiko wa kuishia hatua ya robo fainali.”

SOMA NA HII  KAA KIJANJA WIKIENDI HII UPIGE MAPENE NA MERIDIANBET