Home Simba SC MRITHI WA MIKOBA YA SVEN NI HUYU HAPA

MRITHI WA MIKOBA YA SVEN NI HUYU HAPA


 IMEELEZWA kuwa baada ya mabosi wa Simba kushindwana na Florent Ibenge ambaye ni Kocha Mkuu wa AS Vita pamoja na timu ya Taifa ya Congo kwenye upande wa maslahi sasa wameelekeza nguvu kwa Didier Gomes Da Rosa.

Ibenge alikuwa anatajwa kuwa kwenye rada za Simba kuja kuchukua mikoba ya Sven Vandenbroeck ambaye alibwaga manyanga Januari 7.

Didier anatajwa kujiunga na Simba akitokea katika Klabu ya EL Marreikh ya nchini Sudan ambapo inasemekana kuwa amevunja mkataba wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo.


Hizi hapa timu alizowahi kuzifundisha, 2008–2010 AS Roquebrune Cap Martin, 2010–2010 ES Fos sur Mer
2010–2011 Cagnes-le-Cros, 2012–2013 AS Cannes B
2013–2014 Rayon Sports, 2014–2015 Coton Sport, 2015–2016 CS Constantine, 2016–2017 JSM Skikda, 2017–2018 Ethiopian Coffee, 2019 Horoya AC, 2019–2020 Ismaily na 2020- Al-Merrikh.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara ameweka wazi kuwa mrithi wa Kocha Mkuu, Sven Vandebroeck atatambulishwa mapema kabla ya mashindano ya Simba Super Cup ambayo yanatarajiwa kuanza Januari 27.

“Niwaambie tu kwamba mashabiki wa Simba, kila kitu kipo sawa na mwalimu yupo ambaye ataanza kazi kabla ya mashindano ya Simba Super Cup.
“Mwalimu ana uzoefu na mechi za kimataifa na uzoefu pia wa soka la Afrika hivyo ni suala la muda tu kila kitu kitakuwa wazi,” .
SOMA NA HII  BAADA YA KUANZA 'KUKIWASHA' ...PETER BANDA AFIKIRIWA UPYA SIMBA...PABLO APIGA MAKOFI...