Home news BAADA YA KUANZA ‘KUKIWASHA’ …PETER BANDA AFIKIRIWA UPYA SIMBA…PABLO APIGA MAKOFI…

BAADA YA KUANZA ‘KUKIWASHA’ …PETER BANDA AFIKIRIWA UPYA SIMBA…PABLO APIGA MAKOFI…


KOCHA Mkuu wa Simba Mhispania, Pablo Franco huenda akafanya mabadiliko katika kikosi chake cha kwanza kwa kumtoa kiungo mshambuliaji mmoja na kumuingiza Peter Banda.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumamosi, Pablo amevutiwa na kiwango bora ambacho Banda amekionyesha katika mchezo wa uliopita wa Kombe la FA waliocheza dhidi ya JKT Tanzania.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa, kocha ameshawishika na kiwango bora cha Banda ambacho kimemvutia kumuingiza katika kikosi chake cha kwanza cha timu hiyo.

Viungo hao anaocheza nafasi moja na Banda ni Mghana, Bernard Morisson na Hassan Dilunga ambaye yupo kwenye kiwango bora hivi sasa.

Aliongeza kuwa kutokana na kiwango hicho bora ambacho Banda amekionyesha, Pablo anaangalia uwezekano mkubwa wa kumuingiza katika kikosi chake cha kwanza kiungo mmoja wapo kutoka kati ya Morisson na Dilunga.

“Mchezo wa FA tuliocheza dhidi ya JKT, Banda alionekana kuwa hatari katika goli la wapinzani sambamba na kutengeneza nafasi kadhaa za kufunga mabao.

“Ana uwezo mkubwa wa kukokota mpira na kupiga pasi za mwisho ambazo kama tungekuwa makini, basi tungefunga bao zaidi ya moja.

“Kocha anafikiria kumuingiza katika kikosi chake cha kwanza na kumtoa mmoja wapo kati viungo wawili wa pembeni ambao ni Dilunga na Morisson,” alisema mtoa taarifa huyo.

Pablo alizungumzia hilo hivi karibuni na kusema kuwa: “Nitatoa nafasi kwa kila mchezaji kucheza katika timu yangu, kikubwa ni kuona mchezaji yupi anafaa kuingia katika kikosi changu cha kwanza. Hiyo ni kutokana na ubora wa kila mchezaji aliokuwa nao baada ya kumuona kila mmoja.”

SOMA NA HII  BAADA YA KUSIKIA MANENO YA KUKATALIWA NA MASHABIKI....MUGALU AVUNJA UKIMYA SIMBA...AFUNGUKA YALIYOMSIBU...