Home Uncategorized LUKA JOVIC ALAMBA DILI LA MIAKA MITANO REAL MADRID

LUKA JOVIC ALAMBA DILI LA MIAKA MITANO REAL MADRID

Luka Jovic amejiunga na klabu ya Real Madrid kwa ada ya dau ya Euro milioni 62 amepewa kandarasi ya miaka mitano.

Mshambuliaji huyo ambaye alikuwa akitumikia klabu ya Eintracht Frankfurt ameweza kusajiliwa kwa ada ya dau kubwa kuliko wote ambao wamewahi kusajiliwa klabuni hapo.

Anakuwa mchezaji wa tatu kunuliwa kwa ada kubwa baada ya Cristiano Ronaldo na Gareth Bale.

Bosi wa timu yake ya zamani ya Eintracht Frankfurt, Fredi Bobic amesema kuwa kuondoka kwa Jovic ni hasara kubwa kwao kutokana na mchango wake mkubwa ndani ya klabu
“Kwetu sisi ipo wazi kabisa kwamba tutapata fedha ila bado kuna kitu ambacho tutakikosa kwake, tunamuombea Jovic mafanikio mema katika kuishi ndoto zake, tunajivunia uwepo wake kwetu na uwezo alioonyesha,”amesema.

SOMA NA HII  AZAM FC KUKIWASHA KESHO