Home Uncategorized AZAM FC KUKIWASHA KESHO

AZAM FC KUKIWASHA KESHO

UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa kesho utakuwa na kazi ya kufanya mbele ya Klabu ya Transit Camp kujiweka sawa.

 Mchezo huo wa kirafiki ni maalumu kwa ajili ya Kocha Mkuu, Arstica Cioaba kutazama namna wachezaji walivyopokea mafunzo baada ya kuanza mazoezi Mei 27.Mchezo huo utafanyika Uwanja wa Azam Complex saa 1.00 usiku.

Zaka Zakazi, Ofisa Habari wa Azam FC amesema kuwa kila kitu kipo sawa kwa kuwa wachezaji wamekuwa na morali kubwa ya kufanya mazoezi.

Juni 14 Azam FC itakuwa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbao FC utakapigwa Uwanja wa Azam Complex.

SOMA NA HII  MZAMBIA MAMBO SAFI YANGA, GAZETI LA SPOTI XTRA KATIKA UKURASA WA MBELE LEO JUMAPILI