Azam FC imemtambulisha Dani Cadena, kutoka Hispania kama kocha mpya wa magolikipa klabuni hapo.
Cadena ni kocha wa zamani wa makipa wa klabu za Ligi Kuu Hispania (La Liga) Sevilla na Real Betis.
Kocha huyo pia ameshafanya kazi nchini China na Saudi Arabia, ana uzoefu mkubwa na elimu ya juu ya Shirikisho la Soka la Ulaya UEFA.