Home Habari za michezo MASTAA SIMBA WAANZA KWA MAJANGA MSIMU HUU

MASTAA SIMBA WAANZA KWA MAJANGA MSIMU HUU

Habari za Simba leo

MASTAA watatu wa Simba wameanza kwa majanga msimu wa 2023/24 kutokana na kupata maumivu wakiwa kwenye majukumu yao.
Ikumbukwe kwamba msimu wa 2022/23 Simba ilishuhudia bingwa wa ligi akiwa ni Yanga chini ya kocha Nasreddine Nabi ambaye hatakuwa ndani ya kikosi cha Yanga kwa msimu wa 2023/24.
Yanga kwa sasa ipo chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.
Gamondi atakuwa na kibarua cha kukiongoza kikosi cha Yanga kupambania taji la ligi, Kombe la Azam Sports Federation, Ligi ya Mabingwa Afrika.
Miongoni mwao ni pamoja na Aubin Kramo ingizo jipya kutoka ASEC Mimosas ya Ivory Coast aliyepata maumivu kwenye mazoezi ya timu.
Nyota huyo hajacheza mchezo wowote ndani ya kikosi cha Simba kwenye Ngao ya Jamii pamoja na mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar, uliochezwa Uwanja wa Manungu.
Beki wa kupanda na kushuka Henock Inonga alipata maumivu kwenye mchezo dhidi ya Singida Fountain Gate hatua ya nusu fainali Ngao ya Jamii alipogongana na mshambuliaji Meddie Kagere dakika ya 90.
Mkandaji, Kibu Dennis katika majukumu kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar alipata maumivu dakika ya 75 alikwama kukamilisha dakika 90 nafasi yake ikachukuliwa na Moses Phiri.
Taarifa kutoka Simba kupitia kwa daktari wa Simba Edwin Sportsmed zimeeleza kuwa wachezaji hao wanaendelea vizuri baada ya kupata matibabu.
“Wachezaji wanaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu hivyo kinachoendelea kwa sasa ni ungalizi ili wawe imara kwa ajili ya kuendelea na majukumu yao,”.

SOMA NA HII  PIGA PENATI USHINDE MIHELA YA MERIDIAN BET