Home Habari za michezo AHMED ALLY:- YANGA INAWACHEZAJI BORA SANA…

AHMED ALLY:- YANGA INAWACHEZAJI BORA SANA…

Habari za Michezo

Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema dhamira yao nikuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo wa Derby ya Kariakoo dhidi ya Yanga utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Novemba 5 saa 11 jioni.

Ahmed amesema viongozi, benchi la ufundi pamoja na wachezaji wapo tayari kuhakikisha wanapambana na kupata ushindi na kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo.

Ahmed ameongeza kuwa mchezo utakuwa mgumu hasa ukiangalia ubora wa wapinzani wao ingawa wamejipanga kuwapa furaha mashabiki wao.

“Mechi ya Simba na Yanga huwa ni mechi ngumu huwa haijalishi timu zote zipo kwenye hali gani. Hata mashabiki wa Simba tukicheza dhidi ya mashabiki wa Yanga unaona kabisa amsha amsha jinsi ilivyo.”

“Hata kama Yanga awe vibaya kiasi gani wanaweza wakasafiri na lori kwenda mpaka Mbeya sababu ya kupitia hali ngumu lakini bado wakicheza dhidi yetu mechi huwa ni ngumu.”

“Licha ya kufungwa na Ihefu ambayo imeshazoea kuwafunga Yanga, bado mechi yetu dhidi yao huwa ni mechi ngumu. Na ukiangalia mfululizo wa mechi zao kwasasa unaona kabisa itakuwa mechi ngumu.”

“Lakini tutawafunga sababu sisi Simba tuna wachezaji wenye ubora kuliko wachezaji wao. Yanga wana wachezaji wenye ubora lakini ukiwalinganisha na wachezaji wa Simba, sisi ndiyo tuna wachezaji wenye ubora zaidi kuliko wote.”

“Yanga wana wachezaji wenye ubora kuliko wa Azam, wa Azam wana ubora kuliko Mashujaa na sisi tuna wachezaji wenye ubora zaidi kuliko hao wote, tuna wachezaji wenye ubora wa ngazi ya Afrika. Kama wachezaji wa Simba wakiamua mechi hii tunataka kushinda basi hakuna timu inaweza kutuzuia.”

SOMA NA HII  'UZEMBE' WAKUMRUSU MAYELE AKAFUNGA JUZI WAMGHARIMU INONGA SIMBA...MAKI APANGA KUMPIGA CHINI MAZIMA...