Home Uncategorized MBELGIJI SIMBA AMTAKA KOCHA WA MAKIPA AKASOME, LA SIVYO…….

MBELGIJI SIMBA AMTAKA KOCHA WA MAKIPA AKASOME, LA SIVYO…….


Imeelezwa kuwa Kocha Mkuu wa klabu ya Simba akiwa zake Ubelgiji ameacha maagizo kwa bodi ya klabu ya Simba kuhusu usajili na kuboresha baadhi ya vitu kwenye bechi la ufundi la klabu hiyo.

Kwenye bechi la ufundi Aussems ameitaka bodi kumuongezea mkataba wa mwaka mmoja kocha wake msaidizi Dennis Kitambi ambaye mkataba wa miezi minne umeisha.

Taarifa hiyo pia imeeleza kwenye ripoti hiyo inamtaka kocha wa makipa wa klabu hiyo Mohammed Muharami akasome ili aongeze ujuzi ikishindikana hiyo basi aletwe kocha mpya wa makipa

Aussems kama amepania vile msimu ujao ameitaka bodi ya klabu hiyo iboreshe vifaa vya mazoezi vya klabu hiyo vikiwepo viwanja vya mazoezi na ameiomba bodi ya klabu hiyo ilete mtaalamu wa viungo mpya kutoka nje anayejua aina ya tiba na chakula

SOMA NA HII  BREAKING: SARRI AFUNGASHIWA VIRAGO JUVENTUS