Home Uncategorized MTIBWA SUGAR INA KAZI KWENYE SAFU YA ULINZI, KOCHA HANA MASHAKA

MTIBWA SUGAR INA KAZI KWENYE SAFU YA ULINZI, KOCHA HANA MASHAKA


DICKSON Job, beki chipukizi ndani ya Mtibwa Sugar, Kocha Mkuu Zubeir Katwila amemwani na kumpa mikoba ya kuwa kiongozi wa safu ya ulinzi.
Ikiwa imecheza mechi 29 ambazo ni dakika 2,610 imefungwa mabao 27 ikiwa na wastani wa kufungwa bao moja kila baada ya dakika 96.
Mtibwa Sugar ina kazi kubwa ya kufanyia kazi safu yake ya ulinzi ili kuendelea kuwa bora watakapoendelea pale walipoishia kwenye ligi.
Katwila amesema kuwa wachezaji wake wapo sawa na amewaandaa kisaikolojia kurejea kwenye ubora ili kuendelea kubaki ndani ya ligi.
“Bado tunajua kuna maatizo madogo ambayo yalikuwepo awali ila muhimu ni kuwa tayari kwa ajili ya ushindani, na kupambania nafasi yetu,” amesema.
Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 14 ikiwa imeshinda mechi nane na imefunga jumla ya mabao 22.

SOMA NA HII  BIASHARA UNITED WANA HESABU KALI KWELI