Home Uncategorized BIASHARA UNITED WANA HESABU KALI KWELI

BIASHARA UNITED WANA HESABU KALI KWELI


FRANCIS Baraza, Kocha Mkuu wa Biashara United anaamini kuwa timu yake ina nafasi ya kufanya vizuri ndani ya Ligi Kuu Bara kutokana na mipango makini iliyojiwekea.

Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimamishwa na Serikali kwa muda wa siu 30 na ilikuwa Machi 17 ambapo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliamua iwe hivyo ili kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona.

Timu yake ipo nafasi ya 10 kibindoni ina pointi 40 baada ya kucheza mechi 29 ambazo ni sawa na dakika 2,610.

Imeshinda mechi 10 kama ilivyo kwenye idadi ya sare zake na kunyooshwa mechi tisa ndani ya Ligi Kuu Bara.

Idadi ya mabao ya kufunga ni 21 huku ilifungwa mabao 22 imebakiwa na mechi 9 mkononi kufunga hesabu za msimu wa 2019/20.

SOMA NA HII  LIVE: SHEREHE ZA MAADHIMISHO, MIAKA 56 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR