Home Uncategorized KUMBE ABDI BANDA ALIPOTEZA AMANI ALIPOHISIWA ANA CORONA

KUMBE ABDI BANDA ALIPOTEZA AMANI ALIPOHISIWA ANA CORONA

ABDI Banda, nyota wa Tanzania anayekipinga ndani ya Klabu ya Highlands Parks ya nchini Afrika Kusini na inashiriki Ligi Kuu amesema kuwa aliogopa alipohisiwa kwamba amepata virusi vya Corona.

Nyota huyo alitengwa na timu yake na kuwekwa chini ya uangalizi maalumu wiki iliyopita kutokana na kuonekana akikohoa mara kwa mara jambo lililofanya madaktari wamtenge mbali na wenzake  na kumfanyia vipimo vya Corona.

Baada ya kufanyiwa vipimo vya Corona Banda aligundulika hana Virusi hivyo jambo ambalo limempa amani na anaendelea na shughuli zake kama kawaida kwa sasa.

“Nilipata hofu nilipohisiwa kwamba nina virusi vya Corona ukizingatia kwamba kulikuwa na maambukizi yameshaanza nchini Afrika Kusini, nashukuru Mungu nilipopimwa nilikuwa salama jambo ambalo linanifanya niendelee kuwa na amani.

“Kwa sasa tunachukua tahadhari ya kujikinga na virusi hivi vya Corona ambapo Ligi Kuu imesimamishwa pia hakuna kufanya mazoezi ya pamoja kila mmoja anafanya yeye mwenyewe peke yake ila tunaomba hili lipite maisha yaendelee kuwa vizuri,” amesema.

SOMA NA HII  HIZO REKODI ZA NYOTA WA SIMBA V YANGA NI BALAA TUPU