Home Uncategorized UJUMBE WA JEMBE KUHUSU SHIGONGO

UJUMBE WA JEMBE KUHUSU SHIGONGO


ANAADIKA Saleh Jembe kuhusu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya  Global Group Eric Shigongo baada ya kuteuliwa kuwania ubunge Jimbo la Buchosha jana, Agosti 20:- “Niliposikia Eric Shigongo imetangazwa kuwa wewe ndiye mgombea wa Ubunge jimbo la BUCHOSHA kupitia CCM, nikakukimbia (utaniwia radhi), sikutaka kuiona furaha yako, bila shaka nilijua itaambatana na machozi.
“Najua namna umekuwa na nia ya kuwatumikia watu wa nyumbani kwenu, najua namna ulivyopeleka misaada kwa fedha zako, umenunua vitu vingi sana na hata kuwasaidia wasipokuwa na uwezo wa kulipa ada.

“Wenye vipaji au uwezo wa kufanya jambo umewasimia na wako leo wanajulikana. Uliwahi kununua gari la wagonjwa na haukuwa mbunge na haukuwa katika kampeni za kupata nafasi yoyote Ile.

“HUU ndio WAKATI WAKO, ninaamini CCM na watu wa BUCHOSHA hawatajuta, ninaamini Mwenyekiti wako Rais Magufuli na viongozi wengine hawatajuta na iko siku WATAJIVUNIA SANA wewe.

“Tumeelewana na kupishana mara nyingi sana kikazi na unajua UBISHI Wangu, unajua NISIVYO NA HOFU WALA KUKUBALI KURUDI NYUMA. Lakini mara nyingi umenibadilisha na kunifanya NICHUKUE njia tofauti na nikayaona mabadiliko na baadaye mafanikio.

“Kwa sasa NAJIAMINI sana zaidi ya miaka 10 au mitano iliyopita, ni kiongozi nisiyeyumba wala kukubali kushindwa na mafunzo yako yamekuwa matunda makubwa.

“Kwa walio mbali na wewe ni vigumu sana kukuelewa lakini najivunia bahati ya kufanya kazi KARIBU NA WEWE….

“Naweza kusema Mungu AMEKUSUKUMA ili uwezo wako mkubwa UKAUTUMIE KWA KUWASAIDIA wana Buchosa na WATANZANIA KWA UJUMLA.

“NINAAMINI utashinda Ubunge lakini ninaamini UTAWASHANGAZA wengi kuhusiana na uwezo wako mkubwa kiutendaji hasa katika ubunifu na uamuzi wa kusukuma mambo hata kunapokuwa na ugumu.

“Nikutakie kila la kheri huko mbele, Mungu aendelee kuwa dira kwako.. sisi huku gurudumu LINASONGA… Aluta continua.”

SOMA NA HII  BANDA: MAMBO MAGUMU HATA HUKU SIO BONGO PEKEE