Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA AL AHLY….SIMBA WAANIKA UZI MPYA WA USHINDI MAPEMAAA….

KUELEKEA MECHI NA AL AHLY….SIMBA WAANIKA UZI MPYA WA USHINDI MAPEMAAA….

Jezi mpya za Simba leo

KUELEKEA uzinduzi wa michuano ya Afrika Football League (AFL), uongozi wa Simba umezidi jezi maalum watakazovaa katika mchezo wa ufunguzi wa mchezo wao dhidi ya Al Ahly ya Misri.

Kupitia mzabuni klabu hiyo Sandalans Fashion Wear Limited, leo ametangaza jezi mpya ambazo Simba watazivaa katika mchezo huo unatarajiwa kucheza Oktoba 20, mwaka huu uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Jezi hizo zilizozinduliwa leo  ni rangi mbili, nyuekundu ambayo itavaliwa mechi ya nyumbani na nyeupe itavaliwa  ugenini katika mchezo wa marudiano utakaochezwa nchini Misri.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa jezi hizo, Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Simba,  Salim Abdallah (Try Again) alisema lengo lao ni kuona timu yao inamuonekana mpya katika mashindano mapya ambayo ni mara ya kwanza kucheza.

Alisema ni michuano mikubwa na Simba imefanikiwa kuwepo katika timu nane bora, uzinduzi unafanyika Benjamin Mkapa, mzabuni wetu ameamua kuja na kitu kipya na wachezaji wetu kuwa muonekeano mzuri.

“Sandaland alinihakikishia jezi hizi zinaenda kupiga tena, baada ya uzinduzi huu jezi zimeanza kuuzwa naomba mashabiki kununua ili kuzivaa na kuanza kupendeza.

Naomba mashabiki wanunue na wavae kwa sababu kuna wageni wengi wanakuja na kuona kwamba hapa Tanzania hakuna klabu nyingine zaidi ya Simba,” alisema Try Again.

Alimuhakikishia Mzabuni huyo kutoangusha dhamila yake ndani ya Simba kwa kuifanya timu na mashabiki wake kupendeza kwa jezi mpya katika kila michuano iliyopo mbele yao

Aliongeza na kuwakumbusha wanachama ni vizuri kununuabtiketi mapema kama utaratibu wao ikiwemo kujaza uwanja siku hiyo ambayo inaingia kwa wingi uwanjani kama ilivyo kwa Simba Day.

Naye Mwenyekiti wa wanachama wa klabu hiyo, Murtaza Mangungu alisema nitoe shukrani kwa wote kwenye tukio hili ambao ni zawadi kubwa kwa wanachama na mashabiki wa Simba.

Alisema Simba iko imara na haitayumbishwa na maneno ambayo yanasema na watu kuhusu mashindano hayo kuwa hayakuwa na vigezo ili kuibeza Simba.

“Tutashuhurika nao na wale wote wanaoleta propaganda ya kuiumiza Simba, hatutakubali kuona mtu anayechafua klabu, nawaomba wanasimba kuwa pamoja na kushirikiana na viongozo katika kuifanya Simba inakuwa imara,” alisema Mangungu.

Mkurugenzi  wa Sandalans Fashion Wear Limited,  Yusuf Omary alisema kwa kuwa wanaenda katika hatua kubwa wameona waingia na kitu kikubwa kwa kuleta jezi bora itakayovaliwa kuelekea mchezo dhidi ya Al Ahly.

Alisema mchezo huo utakuwa wa ufunguzi kulingana na ukubwa wa mashundano hayo wameona kuja na kitu bora zaidi kwa kuja na jezi ambazo zitavaliwa siku hiyo.

“Jezi hizo ni bora na tunazindua leo ambazo zitavaliwa katika siku hiyo maalum ya mashindano ya AFL ambayo ni mara ya kwanza kuzinduliwa tena uwanja wa Benjamin Mkapa, Simba ikicheza dhidi ya Al Ahly,” alisema Mkurugenzi huyo.

SOMA NA HII  GOMES AMPA MBINU AME KUPENYA KIKOSI CHA KWANZA MBELE YA ONYANGO