Home Simba SC SIMBA YAPANIA KUFANYA KWELI KWA MKAPA MBELE YA KAIZER CHIEFS

SIMBA YAPANIA KUFANYA KWELI KWA MKAPA MBELE YA KAIZER CHIEFS


KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes , amebainisha wazi kwamba, hajali sana matokeo ambayo waliyapata jana kwenye mechi yao na Kaizer Chiefs kwa kuwa hesabu zake ni kuimaliza mechi hiyo nyumbani.

 

Gomes ameongeza kwamba, kwake matumaini makubwa ya kufanya vizuri katika mechi hiyo ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika yapo katika uwanja wao wa nyumbani ambao wamekuwa na matokeo mazuri sana.

 

Jumamosi, Simba walikuwa na kibarua cha kupambana na Kaizer Chiefs kwenye Uwanja wa  la FNB nchini Afrika Kusini na ilipoteza kwa kufungwa mabao 4-0.


Simba kwenye Uwanja wa Mkapa chini ya Gomes msimu huu, imefanikiwa kuwachapa vigogo Al Ahly, AS Vita, El Merrikh na FC Platinum.


Kocha huyo amesema hesabu zake ni kwenye mechi hiyo ya marudiano na anafahamu wana asilimia kubwa ya kufanya vizuri kutokana na mwendo mzuri wakiwa hapo.

 

“Tuna mechi ya marudiano nyumbani, na hii ni muhimu sana kuweka matumaini kwa sababu tumekuwa tunafanya vizuri hapo.


“Naamini hata mechi hii tutaendelea na hali ileile ambayo tunakuwa nayo kila tunapocheza katika uwanja wa nyumbani,”. 

 

Mabao ya Kaizer Chiefs yalifungwa na Erick Mathoho dakika ya 6, Samir Nurkovic alifunga mawili dakika ya 34 na 57, huku Leonardo Castro dakika ya 63 akihitimisha ushindi huo.Timu hizo zinatarajiwa kurudiana Uwanja wa Mkapa, Dar, Mei 22, mwaka huu.

SOMA NA HII  BENCHIKHA ATANGAZA POINT 15 ZA UBINGWA SIMBA....WENYE TIMU HIZI MJIANDAE...