Home Uncategorized SENZO AMJIBU MOO DEWJI, ATAJA MKATABA WA LUIS MIQUISONE SIMBA SC

SENZO AMJIBU MOO DEWJI, ATAJA MKATABA WA LUIS MIQUISONE SIMBA SC

 

ALIYEKUWA Mtendaji Mkuu Simba, Senzo Mazingisa Mbatha Agosti 20, 2020 amewataka mashabiki wa timu hiyo ya Simba kukubaliana na kile ambacho kimetokea kwa sababu pamoja na yote mpira kwake ni kazi na unaendesha maisha yake.

Mazingisa alisema hayo kutokana na kufahamu kwake kwamba kwa namna moja au nyingine kuachana kwake na Simba huku akijiunga na Yanga ni maamuzi ambayo yamewamuzia mashabiki wa timu hiyo.

 

“Kulikuwa na mambo ambayo yalinifanya kuchukua maamuzi ya kuondoka, kama huna furaha namna nzuri ya kufanya ni kuondoka, sikuondoka kwa ubaya ndio maana niliwatakia kila la kheri.”

 

 

“Nachoweza kusema ni kwamba mashabiki wanisamehe kwa sababu kilichotokea ni sehemu ya maisha kwangu mpira ni kazi, unafanya niendeshe maisha yangu,” alisema Mazingisa.

 

Mtendaji huyo wa zamani wa Simba, amerejea nchini jana akitokea kwao Afrika Kusini kwa mapumziko, “Nimekuja Tanzania kuchukua majukumu yangu mapya kwenye klabu yangu ya Yanga,” alisema.

 

Akijibu kuhusu tuhuma ambazo zimetolewa Agosti 20, 2020 na Mwenyekiti wa Bodi wa Bodi ya Wakurugenzi, Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’ alipohojiwa kwenye kituo cha habari cha Wasafi kuwa hakutimiza majukumu yake ikiwemo kubana matumizi na kuamua kujiuzulu, amesema uongozi ukweli akiwemo Mo Dewji.

 

Senzo amesema alipojiunga na mabingwa hao wa Ligi Kuu mara tatu mfululizo alipanga bajeti na Mo Dewji na bodi nzima na kitendo cha kusema mbele ya umma hajatimiza malengo sio suala la kiungwana.

 

“Sikutegemea iwe hivyo, sipendi kuwe na ubaya baina yangu na waajili wangu wa zamani ni vibaya kuwa hivyo, ripoti yangu ya mwisho kuiwasilisha inaonyesha nimetimiza malengo yangu, nimefanya kile kilichopo kwenye bajeti na hela imepatikana. Ripoti itamuonyesha ukweli wote”

Ameongeza kuwa sio rahisi kwenda kwenye klabu na kuanza kuzalisha hela haraka bali inatakiwa kujenga msingi, kuhakikisha misingi inakuwa vizuri na mifumo yote imekaa sawa kisha msimu unaofata ndio uanze kuingiza hela ila bahati mbaya hakuendelea.

SOMA NA HII  ALIYEELEZWA KUHITAJIKA YANGA APIGWA CHINI KENYA

Senzo amesema Luis ana mkataba wa miaka mitatu na nusu kuitumikia klabu hiyo.

“Ilikuwa shughuli kumpata Luis ila sitazungumzia kuhusu klabu yangu ya zamani ila nitajizungumzia mimi kama niliyehusika kumleta nasema ni mchezaji wa Simba kwa miaka mitatu na nusu” amesema Senzo