Home Habari za michezo RASMI…LIGI YA BONGO SASA KAMA MBELE TU…WACHEZAJI KULIPWA VIINUA MGONGO WAKISTAAFU…

RASMI…LIGI YA BONGO SASA KAMA MBELE TU…WACHEZAJI KULIPWA VIINUA MGONGO WAKISTAAFU…


Wachezaji 640 wa timu za Ligi Kuu Bara, maofisa wa benchi la ufundi na familia zao watapatiwa bima za afya zitakazowawezesha pia wachezaji kupata kiinua mgongo wanapopata ajali kuanzia jana.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC inayogharamia bima hizo kwa kushirikiana na kampuni za Britam na Sanlam, Theobald Sabi alisema sambamba na hilo, pia bima hizo zitawarahisishia kupata huduma bora za afya wanapoumwa au kupata majeraha.

Sabi alisema bima hizo zitasaidia kuwapa wachezaji uhuru wa kuonyesha vipaji bila hofu. “Huduma hii itawapatia wachezaji uwezo wa kupata matibabu bora ndani na hata nje ya nchi pale itakapobidi. Zaidi pia kupitia huduma hii wachezaji watapata mafao ya kipato pindi mchezaji atakapopata madhara ya kudumu au kupoteza maisha,” alisema.

“Faida nyingine ni pamoja na wahusika kupata fao la kiinua mgongo pindi watakapopata ajali na kushindwa kuendelea na mchezo wa soka.”

Rais ws Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia alisema hatua hiyo ni ya kihistoria na inaunga mkono mkakati wa shirikisho na serikali kukuza soka nchini.

“Kwa hatua hii ya leo nadiriki kusema Benki ya NBC si tu ni mdhamini wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, bali pia ni mshirika muhimu katika kukuza mchezo. Kwa muda mrefu tumekuwa tukipata changamoto za kiafya kwa wachezaji wetu,” alisema.

“Na suala zima la matibabu limekuwa changamoto kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ukata unaozikabili klabu nyingi hapa nchini. Kupitia huduma hii tunakwenda kumalizana na changamoto hii.”

Kutokana na ukata, timu nyingi zimekuwa zikishindwa kugharimia matibabu wachezaji wao hasa yale makubwa.

Suala hilo limekuwa kilio cha wadau wa michezo kwa muda mrefu, hata hivyo jambo hili likitekelezwa litaifanya ligi ya Tanzania kuwa miongoni mwa ligi chache Afrika ambazo wachezaji wake wanabima za afya.

SOMA NA HII  KAIZER CHIEF WAIZIDI UJANJA SIMBA KWA STARIKA LA MAGOLI KUTOKA CAMEROON...'WAINGILIA TREN KWA MBELE'...