Home Habari za michezo SAKHO AZALIWA UPYA SIMBA….KWA HILI ANALIFANYA ‘HUYU DOGO’..YANGA MSAHAU UBINGWA…

SAKHO AZALIWA UPYA SIMBA….KWA HILI ANALIFANYA ‘HUYU DOGO’..YANGA MSAHAU UBINGWA…

Habari za Simba

Winga wa Simba, Pape Ousamane Sakho amekuwa akifunga mabao mengi kwa mashuti makali, lakini kumbe mishuti hiyo anaifanyia kazi mazoezini na jana alikiwasha na kuwa gumzo kwa mashabiki waliohudhuria mazoezi hayo.

Sakho ambaye mwaka jana alipata tuzo ya bao bora la mwaka Afrika, jana alionekana kupiga mashuti makali mazoezini ambayo mengine yalikuwa yakigonga mwamba na kurejea uwanjani.

Kipa Beno Kakolanya ndiye aliyekuwa akionja joto ya mashuti ya Sakho na mara nyingi alipangua, mengine yalizaa mabao na mengine yaligonga mwamba.

Katika mazoezi yaliyofanyika jana asubuhi kwenye Uwanja wa MO Simba Arena Bunju Sakho, Agustine Okrah na Sawadogo walionekana kuwaka zaidi. Baada ya kocha msaidizi Ouanane Sellami kugawa vikosi viwili na kucheza mechi ya nusu uwanja wachezaji hao walifanga vizuri zaidi.

Sawadogo ambaye amesajiliwa hivi karibuni alianza mchezo uliopita dhidi ya Dodoma na kufanya vizuri na ameendelea kufanya vizuri hata mazoezini jana kutokana na pasi zake safi zilizofika kwa wenzake na kukaba kwa akili.

Kwa upande wa Okrah ndiye mchezaji aliyeongoza kufunga jana akiwa amefunga mabao matatu Chama, Onyango nao hatari

Kabla ya kuanza mazoezi ya kuchezea mpira, kocha Sellami aliwataja wachezaji wote kukimbia kwa kuzunguka uwanja na zoezi lililofanyika kwa dakika 10 na baadaye kugawa makundi manne yenye wachezaji watano hadi sita na kuwataka kukimbia kwa kasi kutoka goli moja hadi lingine.

Katika zoezi hilo likilodumu jwa dakika 15, Chama na Onyango walionekana kumudu zaidi kwa kuwa wa kwanza kila wakati na kupigiwa makofi na kocha huyo.

Hivi karibuni Chama alizua mjadala kwa mashabiki baada ya kocha mkuu Robertino Oliveira kumtoa dakika ya 30 katika mchezo dhidi ya Mbeya City huju wengi wakidai hakustahili kutolewa.

Kocha Oliveira alisema alimtoa mchezaji huyo mapema kwa madai hakuwa na kasi uwanjani na alicheza taratibu tofauti na alivyokuwa anataka wachezaji wacheze kulingana na mechi hiyo.

Saido, Boko wakosekana mazoezi

Wachezaji wawili, John Bocco, Said Ntibazonkiza ‘Saido’ ndio pekee hawakuwepo katika mazoezi jana. Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu alisema wachezaji hao wana ruhusa na leo wanaweza kujiunga na timu.

Akizungumzia mazoezi hayo kocha Mgunda alisema: “Tunaendelea na mazoezi kujiandaa na mechi dhidi ya Coastal, itakuwa mechi ngumu kwa sababu wapinzani wetu hawana matokeo mazuri katika mechi mfululizo hivyo lazima tujipange vizuri kuwakabili.

” Nafurahi kuona wachezaji wote wanapambana mazoezini na hiyo inaonyesha kuwa wana hamu ya kufanya vizuri katika michezo yote iliyo mbele yetu, ” alisema Mgunda na kuongeza.

“Bado ubingwa upo wazi kwani kwani kwenye soka lolote linaweza kutokea, lazima upambane kama mwanajeshi , hakuna kukata tamaa hadi mwisho.”

SOMA NA HII  HIVI NDIVYO YANGA YA GSM WALIVYOPINDUA MEZA KIBABE USAJILI WA PHIRI...SIMBA WABAKI WAKILIA...